Correspondance Course - Lesson 22

SOMO LA 22

DHAMBI NA MATOKEO YAKE (SEHEMU YA 1)

SOMO: Mwanzo 2 na 3

Dunia iko katika hali mbaya: vita, njaa, magonjwa, vurugu, mauaji, mateso n.k. Lakini, Mungu aliiumba dunia ikiwa ‘njema’. Mwanadamu ameichafua! Hulka ya mwanadamu ya uchoyo, ubinafsi, wivu na kutotii-mamlaka vimeiharibu jamii na dunia hii.

Yalianzia wapi ‘kwenda mrama’?

Hapo mwanzo Mungu alimuumba mwanadamu wa kwanza, Adamu. Adamu aliumbwa kutokana na mavumbi ya nchi:

“Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya nchi, akampulizia puani pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi hai” (Mwanzo 2:7).

Mungu aliweka bustani nzuri kwa ajili ya Adamu kuishi humo, na baada ya hapo akampatia mke aliyemwita Hawa. Adamu na Hawa hawakuonesha kama wangemtii Mungu au la mpaka walipojaribiwa. Mungu alikuwa amewapa amri moja ndogo:

“Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika” (Mwanzo 2:16,17).

Adamu na Hawa walikuwa na uchaguzi

Wangeweza kumtii Mungu, au kutomtii na kula tunda la mti uliokatazwa. Walikuwa huru kuchagua. Mungu hakuwa ametengeneza watu walio kama mashine, wasioweza kuchagua kama watii au wasitii. Mungu alitaka wawe watu wanaoweza kuichagua njia yake kwa sababu ya kumpenda na kumheshimu.

Nyoka alikuja na kuwadanganya. Nyoka aliwaambia kuwa wasingekufa kama wangekula tunda lililokatazwa, na kwamba badala yake wangekuwa kama Mungu, wakijua mema na mabaya. Adamu na Hawa walitaka kuerevuka; kufanana zaidi na malaika. Walichagua kulila hilo tunda, na kwa kufanya hivyo walifanya dhambi kwa kutomtii Mungu.

Adhabu

Mungu alikuwa amewaambia wangekufa kama wasingemtii. Kwa hiyo Adamu na Hawa walihukumiwa kifo, na kutimuliwa watoke katika bustani ya Edeni. Ingawa waliishi maisha marefu baada ya hapo, walibadilika na kuwa viumbe vinavyokufa. Walikuwa sasa wakichoka, wakiugua, wakizeeka na hatimaye kufa, kama ilivyo sasa kwako na kwangu.

Kifo ni nini?

Kifo kilikuwa ni adhabu kwa sababu ya dhambi. Mungu alikuwa amesema:

“U mavumbini wewe, nawe mavumbini utarudi” (Mwanzo 3:19).

Kwa hiyo mwili wa Adamu ulioza alipokufa na aliyarudia mavumbi, ambayo ndiyo yaliyokuwa yametumika kuufanya huo mwili. Mavumbi ni udongo. Mungu alimuumba Adamu kutokana na udongo wa nchi, na baada ya hapo alimpulizia pumzi ya uhai, kabla hajawa ‘nafsi hai’:

VUMBI + PUMZI YA UHAI = NAFSI HAI

Adamu alipokufa, ilikuwa ni:

NAFSI HAI – PUMZI YA UHAI = NAFSI ILIYOKUFA

Kwa hiyo tunaona kuwa:

NAFSI HAI ukitoa PUMZI YA UHAI ni VUMBI (udongo)

Hakuna sehemu ya Adamu iliyokwenda kuishi mbinguni alipokuwa amekufa; kwa hakika hakuna! Mauti yake yalikuwa ni adhabu ya Mungu kwa ajili ya dhambi, na kifo maana yake ilikuwa mwisho wa uhai wote; mwisho wa kuishi. Kifo cha Adamu hakikuwa na utofauti wowote na chetu. Sisi wote tunafanya dhambi, kwa hiyo sote tunakufa:

“Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi” (Warumi 5:12).

Hili halina maana kwamba, watu wote ni wauaji au wazinzi au waongo. Mawazo yasiyo ya wema, yenye ubaya: kiburi, choyo, hasira n.k (ambayo ni udhaifu wetu wote wa kila siku), yote ni dhambi machoni pa Mungu. Hakuna kati yetu atakayekwenda mbinguni tukifa.

Hakuna chochote kinachoitwa ‘roho’ kisichokufa

Hakuna mahali ambapo Biblia inataja uwepo wa ‘roho’ isiyokufa. Hakuna kitu kinachoendelea kuishi mtu anapokuwa amekufa. Hakuna cheche ya uhai ya kimbingu isiyozimika katika mwanadamu anapokufa.

‘Roho’ ni uhai; kiumbe hai, au mtu, au nafsi

Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya vifungu vilivyopo katika Biblia inayoonesha sehemu neno hili ‘roho’ linapotumika. Hebu uvitazame mwenyewe uone kama utakubaliana na maoni yaliyotolewa:

REJEA

                          MAONI

Mwanzo 46:15

 

 

Mwanzo 46:26

 

 

Walawi 5:2

 

 

Walawi 17:12

 

 

Yoshua 10:28, 30,32, 35, 37

 

 

Yoshua 11:11

 

 

Matendo 27:37

Wana wa Yakobo (wanaoishi) wanaitwa ‘nafsi’ (kwa Kingereza-souls); lenye maana ya ‘roho’.

“Nafsi zote” (all souls) hapa kwa hakika inamaanisha “watu wote”.

“Kama mtu akigusa kitu kilicho najisi …..” -neno ‘roho’ (soul) hapa ndilo lililotafsiriwa ‘mtu’.

“Kama mtu akifanya dhambi, na …..” (ms. 17): Neno ‘roho’ (soul) hapa ndilo lililotafsiriwa ‘mtu’.

Maana ya roho ni mtu. Roho (souls) zinaweza kufanya dhambi, kwa maneno mengine watu wanaweza kufanya dhambi.

  “…….Hapana mtu mingoni mwenu aliye na ruhusa kula damu…..” (ms. 12).

Neno ‘roho’ (soul) hapa ndilo lililotafsiriwa ‘mtu’.

Hapana mtu (‘roho’ yaani mtu) kati yao aliyekuwa akiruhusiwa kula damu.

Neno wote katika mistari hiyo limekaa badala ya ‘roho wote pia’ (All the souls).

‘Roho wote’ (yaani, watu wote) waliangamizwa kabisa. (‘Roho’ wanaweza kuangamizwa, kuuwawa!)

Neno ‘wote’ tena ni neno ‘roho’.

“Wao wakawapiga wote pia waliokuwamo….”

(And they smote all the souls that were…..)

Waliwaua roho wote (watu wote); hakuna aliyebaki akipumua.

“Na sisi tuliokuwa ndani ya merikebu tulipata watu 276”

Neno ‘watu’ hapa ni neno ‘roho’.

Roho 276 ni watu 276.

(“And we were in all in the ship 276 souls”)

Roho hapa ni wazi ni hao abiria.

Kuna mifano mingi zaidi tungeweza kutoa kuonesha kuwa neno ‘roho’ maana yake ni mtu (au kiumbe hai). Ni neno pia linalotumika kuwahusu wanyama katika lugha ya asili (lugha ya Kiebrania). Kwenye Mwanzo 1:21, 24, 2:19, 3:10 ni neno lililotafsiriwa ‘kiumbe hai’ kwenye Kiswahili. Kwenye Kingereza ni ‘living creature’. Yote haya yanathibitisha kile kinachosemwa katika Mhubiri:

“Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama, jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu, naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili. Wote huenda mahali pamoja, wote hutoka katika mavumbi, na hata mavumbini hurudi tena” (Mhu. 3:19, 20).

Hakuna utofauti wowote kati ya mtu na mnyama katika mauti. Mnyama hana sehemu inayokwenda mbinguni anapokufa, na mwanadamu ni hivyo hivyo. Wote wanakuwa ni miili isiyokuwa na uhai wanapoacha kupumua; ni udongo:

“Roho” maana yake ni uhai, mtu, kiumbe kilicho hai

Vifungu hivi vinatuonesha kinachotokea tunapokufa:

Zaburi 146:4

 

Mhubiri 9:5

Zaburi 6:5

 

Zaburi 39:13

Zaburi 115:17

“Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, siku hiyo mawazo yake yapotea”

“Wafu hawajui neno lolote……….”

“Mautini hapana kumbukumbu lako, katika kuzimu (kaburi) ni nani atakayekushukuru?”

“Uniachilie nikunjuke uso, kabla sijaondoka nisiwepo tena”.

“Sio wafu wamsifuo BWANA, wala wowote washukao kwenye kimya” (kaburini).

Vifungu hivi vyote vinaonesha kuwa, watu waliokufa hawana utambuzi wowote; hawawezi kufikiri.

Mfalme Hezekia alipoambiwa kuwa alikuwa afe, alisononeka sana. Alitaka aendelee kuishi kwa kuwa alijua kwenye mauti hakukuwa na kitu. Alimwomba Mungu aishi, ili aweze kuendelea kumsifu:

“Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako” (Isaya 38:18).

Badala yake, anamwambia: “Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo” (ms.19).  

Je, mfalme Daudi? Tunaambiwa wazi mfalme Daudi hakwenda mbinguni, ingawa anaitwa mtu aliyekuwa na moyo uliompendeza sana Mungu (Matendo 2:34, 13:22)

Watu wote wapo kwenye hukumu ya kifo kwa sababu ya dhambi. Hawaendelei kuishi kwa namna yoyote nyingine baada ya kufa.

Kama hatulielewi hili vizuri, hatuwezi kamwe kutambua jinsi ambavyo Bwana Yesu alivyoteseka na kufa ili kutuweka huru na matokeo ya dhambi.

Kama tungekuwa na ‘roho zisizokufa’, kusingekuwa na haja ya Yesu kutufia. Biblia inatuambia, hakuna tumaini la uzima kama sio katika Kristo.

Muhtasari

  1. Mungu alimuumba Adamu kutokana na mavumbi ya nchi.
  2. Alimfanya aweze kuishi kwa kumpulizia pumzi ya uhai katika pua zake.
  3. Mungu alimpa Adamu amri. Alimwambia kwamba kama akiivunja amri yake, adhabu yake itakuwa kifo.
  4. Adamu na Hawa hawakumtii Mungu; waliivunja amri yake. Matokeo yake wakawa viumbe vinavyokufa.
  5. Watu wote wanatokana na Adamu, na wanairithi hulka yake ya dhambi. Watu wote wanakosa na wanakufa.
  6. Neno ‘roho’ linamaanisha uhai au kuwa hai, na kwa kawaida linatumika kwa mtu.
  7. Msemo ‘roho isiyokufa’ haupo kwenye Biblia.
  8. Kifo ni adhabu na matokeo ya dhambi (sio ‘Mungu kukupenda zaidi’).
  9. Hakuna sehemu ndani yetu au kitu kinachoendelea kuishi tunapokufa.

Kifungu cha kusoma: Mhubiri 9

Mstari wa kujifunza: Zaburi 146:4

“Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, siku hiyo mawazo yake yapotea”.

 

Swahili Title: 
Dhambi na matokeo yake (Sehemu ya 1)
Swahili Word file: 
PDF file: