Exploring the Bible Course - 23

MTUME PAULO AENEZA INJILI KATIKA ULIMWENGU WOTE WA KIRUMI.

SOMO LA 23 SOMO MATENDO 13-28

 

Katika matendo 9 tulitafakari kugeuzwa kwa Sauli ambaye baadaye aliitwa Paulo.Pale tuliona kwamba Bwana alimtaja kuwa “yeye ni chombo changu kiteule kitakachobeba jina langu mbele ya watu wa mataifa, Wafalme na Watoto wa Israel (aya ya 15) sasa tutaona jinsi kazi hii ilivyofanyika.

 

SAFARI ZA PAULO ZA KIMISSIONARI.

Katika Matendo ya Mitume safari tatu za Paulo zimeelezwa. Tunaposoma habari zake twaelewa jinsi injili ilivyoenea katika Dola ya-kiRumi kadiri jumuiya za Waumini zilivyozidi kukua katika Majiji mbalimbali ya Dola tunaweza kuelewa kwa nini Paulo alihitaji kuwaandikia barua hizi ziliandikawa ili ziwatie moyo katika Imani,kujibu maswali yao na kurekebisha matatizo yaliyo jitokeza miongoni mwao.

 

Baadhi ya barua hizi zimehifadhiwa kwa uwezo mkubwa wa mwenyezi Mungu ili kwamba tunufaike na mafundisho ya Paulo yaliyo husishwa kwa kutuongoza hadi leo.

 

Neno la Kigriki lenye maana ya kila jumuiya ya Warumi ni Eklesia inayotafsiriwa”Kanisa”katika Biblia zilizo nyingi zaidi.Neno hilo ni muungano wa EKLESIS, litokanalo na “Kalea” yaani “Kuita”na herufi zilizo tangulia ek yaani “tokana na”linaeleza mkusanyiko wa watu walioitiwa kutokana na wengine kwa shabaha maalum Neno hili linaonyesha kwa usahihi kuwa waumini ni jumuiya ambayo iliitwa (iliteuliwa) na Mungu kwanjia ya mafunzo ya injili kukaa pembeni na mienendo ya ulimwengu na kumfuata(1Petro 2:9;Matendo) (15:14 Waefeso 1:18,4:4).

 

SAFARI YA KWANZA (MATENDO 13-14)

Tunaposoma sura hizi twaweza kufuata njia ya Paulo na Barnaba Kypro kwanza halafu Galatia jina lake la Uturuki ya kati ya sasa,Biblia zilizo nyingi zenye ramani nyuma zitakuwa zinazoonyesha safari hizi.Baadaye Paulo aliandika “waraka wake kwa Wagalatia”kwa waumini walioishi katika eneo hili.

 

SAFARI YA PILI (MATENDO 16-18)

Katika safari hii Paulo na Silas walizuru tena Eklesia ya Galatia na kuendea hadi Troa na kuvuka hadi Filipi na kushuka Athene na halafu kuendelea hadi Karinto.Safari ya kurudi Yerusalemu iliwapitisha Efeso halafu kwa meli hadi Yudea.Baadaye Paulo aliandika nyaraka kwenda kwa wale aliokuwa amekutanana katika safari hii hizi ni nyaraka kwa Wafilipi,Wathessalonike, na Wakorinto.

 

SAFARI YA TATU (MATENDO18-21)

Kwa mara nyingune Paulo alisafiri kupitia Galatia na kuendelea hadi Efeso ambapo alikaa miaka mitatu. Kutoka hapo injili ilsambaa hadi “Asia” yote ikasikia neno la Bwana aliendelea hadi Ugiriki kabla ya kurudi Yelusalemu.Baadaye Paulo aliandika nyaraka kwa Waefeso na Wakolosai(ikiwa ni pamoja na barua ya binafsi kwa Filemoni).

 

KUFUNGWA KWA PAULO YERUSALEMU NA SAFARI YA ROMA

(Mat 21-28).

Paulo aliporejea Yerusalemu baada ya safari ya tatu alikamatwa ndani ya Hekalu na viongozi wa dini ya Kiyahudi na baadaye kuwekwa chini ya ulinzi na waumini.Kwanza alifungwa Yerusalemu,halafu kaizari alipelekwa Rumi.Safari yake ilikuwa ya hatari sana lakini hatimaye aliwasili Rumi salama na kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani.Japo alikuwa amefungwa minyororo.

aliweza kuandika kwa mkono wake au kwa imla barua ambazo zilikuwa za manufaa makubwa kwa jumuiya za waumini za awali na zasasa.

 

UWEZA ULIOMHAMASISHA PAULO.

Tunapo angalia sehemu ambazo Paulo alitembelea alipokuwa anasafiri katika Himaya yote na katika safari yake ya mwisho Rumi tunaona kwamba yeye,kuliko wengine wote, ndiye aliyehusika katika uenezaji wa Injili kwa watu wa Mataifa.

 

Katika baadhi ya maandiko yake tunaona japo kwa mbali nguvu ilivyomwezesha kujitolea kufanya kazi nzito kama ile.

 

Alisema,katika Waraka wake kwa Waumini.Kwa hiyo,kwa nguvu niliyonayo niko tayari kufundisha Injili kwenu nyiye niliokopia.Kwa sababu sionei haya Injili ya Kristo.Kwakuwa ni nguvu ya Mungu ya Wokovu kwa kila aaminiye kwa wachache kwanza na pia kwa Wagiriki(Warumi 1:15-16)

 

Tena akaandika (“Tuna Moyo uleule wa imani kama ulivyoandikwanandiyo maana nimesema.Sisi pia tunaamini na ndiyo maana tunasema (Wakorinto 4:13)

 

Paulo aliamini kuwa ujumbe ukomo ndani ya Injili ndilo tuaamini pekee la Mwanadamu kiasi kwamba aliamini sana alilazimika kuuzungumzia kwa kila mtu aliyepatana naye.

 

Kwa kweli ametuachia sisi mfano mzuri wa kufuata.Kama kweli tunaamini Injili basi tusiishie kuitii katika ubatizo na kutembea kwa utiifu mbele za Mungu bali tulazimike kuizungumzia kwa wengine ili nao washiriki katika tumaini kuu la wokovu.

 

 

BARUA NYINGINE ZA AGANO JIPYA.

Kama tulivyosema,barua zilizo nyingi zilizomo katika Agano jipya ziliandikwa na Paulo kwa jumuiya ya Waumini.Paulo pia,aliandika barua za binafsi kwa baadhi ya wale ambao walifanya naye kazi kubwa kama vile Timotheo,Tito na Filemoni.Japo hakuna mwandishi mahususi aliyetajwa barua kwa Waebrania inahusishwa na wasomi walio ewngi, na Paulo.

 

Wafuasi wa Yesu wengine pia waliandika barua ambazo zimo ndni ya Agano jipya.Hizi ni barua za Yakobo,Petro, Yohana naYuda.

 

Barua hizi siyo tu zinatusaidia kuelewa yaliyo ya lazima kwa wokovu wetu bali pia zinatoa mwongozo kwa wafuasi ili waweze kumtukuza Mungu katika maisha yao.

 

ROHO MTAKATIFU KATIKA KARNE YA KWANZA

Kama tulivyokwishaona Bwana Yesu Kristo alikuwa amepewa uwezo wa Roho Mtakatifu kufanya miujiza ili yasiwepo mashaka kwamba alituma na Mungu (Yohana 3:2; Matendo 2: 22; ona Somo la 20).Baada ya ufufuo wake Yesu aliwaambia wafuasi wake kuwa atakapokuwa ameondoka kwenda Mbinguni wao pia wangepokea Roho Mtakatifu pia alieleza ni kwa nini iwe hivyo.Nguvu hiyo ilitolewa kwa sababu mbili muhimu.

 

 1. Ingewapa uwezo wa kuelewa njia ya Mungu vizuri zaidi na kuwawezesha kukumbuka yale yote aliyofundisha Yesu (Yoh 14:26)

 2. Wangewezesha kufanya miujiza kwa jina la Yesu kama ishara isiyokanushaka wamba alikuwa amefufuliwa katika wafu na kwamba Mungu alikuwa anatetea injili waliokuwa wanatangaza.Mungu asingeshuhudia kwa miujiza kwa ujumbe wa wahubiri kama wasingekuwa wanasema kweli.(Yohana 9:30-33).

 

Ni kwa nguvu za Roho mtakatifu ndipo wafuasi wa Yesu walipoweza kuweka kumbukumbu za mafundisho ya Yesu kwa usahihi.Kabla ya kifo cha Yesu wafuasi maranyingi walishindwa kuelewa mafundisho yake lakini baada ya kifo chake,Roho Mtakatifu aliwawezesha kuweka kumbukumbu sahihi za yale waliyoona na kusikia.

 

MIUJIZA

Kwa Watu ambao leo wanadai kuwa wanauwezo wa Roho Mtakatifu na wanaweza kufanyamiujiza kama Mitume walivyo fanya katika barua ya kwanza.Huu ni udanganyifu. Tunaposema maisha ya Yesu naya Mitume tunatambua haraka kuwa matokeo ya miujiza yalikuwa ya papo kwa papo na kamili kila mara walikuwapo mashahidi walisoma ambao walizungumzia maajabu ya miujiza walioona ili kwamba makundi ya Watu walisafiri mamia ya kilometa kuja kuponeshwa (Mathayo 4:23-25)

kwanjia hiyo hiyo miujiza iliyofanywa naMitume kwa jina la Yesu ilitangazwa na kufika mbali (Matendo 4:16:5:14-16)ushuhuda haukuishia kwa waumini wa Kidhehebu Fulani kidogo.

 

Leo wafuasi wa imani mbalimbali za kidiniwanadai kufanya miujiza kwa uweza wa Roho Mtakatifu.Ukweli kwamba imani zao zinatofautiana,uanhihirisha kuwa hawafanyi miujiza kwa jina la Mungu. Kwa kuwa Mungu anajinadi kama Mungu wa kweli.Miujiza lazima imtukuze Mungu na kwahiyo ni lazima ishuhudie ukweli wa Injili kama ilivyo kuwa katika karne ya kwanza ni lazima kwanza tuchunguze mafundisho ya wale wanaodai kuwa wana uwezo huo,ili tuweze kuona kama kweli yana kubaliana na Biblia (1Yohana 4:1)

 

Roho Mtakatifu alitolewa katika karne ya kwanza ili Yesu kwanza na halafu Mitume wapate ushuhuda waki Mungu kwa kweli wa mambo aliyohubiri.Agano jipya lilipoandikwa na watu wakaweza kusoma maajabu ya Yesu Kristo na mafundisho ya mitume haikuwa tena lazima Mungu hakutaka tena Mitume watumie uweza wake baada ya Mitume na wafuasi wao wa karibu kufariki dunia. Hadi wakati huo ujumbe wa Injili ulikuwa umeishaenea katika Asia Ulaya na Afrika ya Kaskazini na nakala za mahubiri hayo zilikuwa zimeisha unganishwa kuwa kitabu kiitwacho Agano Jipya.

 

Mtume Paulo alipotambua kuwa hili lingetokea alizungumzia wakati ambapo uwezo wa kutabiri,kusema lugha za kigeni n.k. ungekoma,kwa sababu utashi wa Mungu uliofunuliwa ungekuwa umeandikwa wote katika Neno lake,Biblia (Wakorinto 13:8-10)

 

Kusema katika Lugha mbalimbali

Katika Matendo 2 tuna kumbukumbu

 

Ya Mitume “kuzungumza katika lugha mbalimbali “ Tunaposoma kisa hiki tunaona kwamba kulikuwa na Wayahudi waliokusanyika kutoka sehemu zote za Mashariki ya kati na bado mitume walipozungumza “Kila moja aliwasikia katika Lugha yake mwenyewe”(aya ya 6).

Muujiza huu wafanya watu wastaajabu na kusema “Tazama hawa wote wanaozungumza si Wagalilaya? Na inakuwaje sisi wote tunawasikika katika lugha zetu tulizozaliwa nazo?

(aya ya 7-8)

 

Muujiza wa kuzungumza katika lugha nyingine uliwezesha kuenea haraka zaidi kwa Injili katika dola yote. Mitume ambao walikuwa Wagalilaya sasa waliweza kusema lugha za kigeni kufanya hivyo kuliwawezesha kuhubiri Biblia Dunia nzima katika lugha ya wasikilizaji.Injili ilipoaminika na kukubalika katika nchi hizo hapakuwa na haja ya muujiza huu kuendelea.

 

 

KITABU CHA MWISHO CHA BIBLIA –UFUNUO.

Kitabu hiki cha mwisho kimewastaajabisha wengi wanaotaka kuelewa Biblia.Ufunuo ulitolewa kwa Mtume Yohana alipokuwa mfungwa katika kisiwa cha Patmos wapata mwaka wa 96

baada ya Kristo.Wengi wanatamani kukielewa kitabu hiki kabla hawajajua yaliyotanguliwa kuna jambo moja la msingi ambalo mara nyingi walikosa.

 

UFUNUO ULITOLEWA NA YESU KRISTO

Kuwaonyesha watumishi wake ambao ni lazima yatokee katika muda mfupi ujao”kwa hiyo ni kitabu cha unabii inachoonyesha mambo ambayo ni lazima yatokee katika muda mfupi ujaokwa hiyo kimekuwa kitabu cha kutia Moyo kwa watumishi wake katika kila kizazi tangu wakati wa Yohana hadi leo.

 

Ni kitabu cha ajabu kwa jinsi ya usahihi wa utabiri wake,hata hivyo kinaweza kueleweka tu kama msomaji anao mwanga wa maandishi ya Biblia na ujumbe wakinabii hasa ya Daniel ambayo yalikitangulia.Kujaribu kukielewa bila msingi huo kutasababisha mkanganyiko na makosa.Kilitolewa mahsusi kwa watumishi wa Kristo ambao wameishaelewa matakwa na makusudio ya Mungu kuhusu Dunia kufikiria maono yake na ujumbe kwa subira na uangalifu ni njia ya kuwatia Moyo wale wote wanaofanya jitihada ya kukisoma.

 

Ujumbe wa ufunuo unakubaliana kabisa na Biblia nzima unatangaza fundisho la Ufalme wa Mungu atakaokuja duniani.

 

 • Falme za Dunia hii zimekuwa falme za Bwana wetu na Kristo wake na atazitawala milele”(Ufunuo 11:15)

 • Umetufanya wafalme na makuhani mbele ya Mungu wetu na kutawala Duniani (Ufunuo 5:10)

 • Tazama, nakuja haraka; na tuzo yangu ninayo, kumpa kila mtu kulingana na kazi yake (Ufunuo 22:12)

 

Yohana anamalizia kitabu hiki kwa Sala ya dhati ni Sala ya wale wote ambao kwa uaminifu wanatarajia kuja kwa Bwana, Yesu Kristo tunayo kila sababu kuamini kuwa karibu atarudi kuwatunza wale ambao wamejitahidi kumtumikia na wamesali kwa dhati “Ufalme wako ufike lifanyike duniani kama Munguni “(Mathayo 6:10) sote tujiande kwa siku hiyo kwa njia iliyochagua ili sisi pamoja na Yohana tuweze kusali kwa haki kabisa “Hata hivyo,njoo,Bwana Yesu (Ufunuo 22:20)

 

MUHTASARI

 

 • Kitabu cha Matendo kinatupa undani wa safari za Mtume Paulo aliposari katika dola nzima ya Rumi akihubiri Biblia dola nzima ya Rumi akihubiri Biblia

 • Kitabu Ufunuo kilitolewa na Yesu mbinguni mahsusi kwa Mtume Yohana kwa manufaa watumishi wa Kristo tangu wakati wa Yohana hadi leo (Ufunuo 1:1-3) sehemu kubwa ya kitabu hiki ni unabii na kinatoa miongoni mwa mengine, mtiririko wa matukio katika Ulaya na Mashariki ya kati tangu mwaka 96 baada ya Kristo hadi ufalme wa Mungu utakapowekwa hapo duniani chini ya utawala wa Yesu Kristo (Ufunuo11:15-18) kwa huyo kimetupa sura ya kinabii ya mambo yanayotokea hapa siku hizi kuelekea kurudi kwa Yesu na kinatuasa jinsi tunavyotakiwa kujitayarisha kwa ajili ya tukio hilo (Ufunuo16:15)

 • Hata hivyo,njoo Bwana Yesu “(Ufunuo22:202) ni sala ya dhati ya wale wote ambao baada ya kuelewa mpango Mtukufu ambao Mungu ametufunulia katika Injili wameamini,wakabatizwa katika jina la BwanaYesu Kristo na wanajitahidi kumtukuza mungu katika maisha yao.(Marko15:15-16)

 

 

SOMO LA 23. MASWALI

 

  1. Paulo alitumwa kwa nani hasa na Injili?

  2. Katika kigiriki cha Agano jipya neno ekklesia linatumika kuzungumzia jumuia za waumini kwanini neno hili lilitumika kuwaeleza waumini?

  3. Ni safari ngapi za kimissionari allizofanya Paulo ambazo zimeandikwa?

  4. Ni uweza gani uliomsukuma Paulo kuhubili Injili hata kuhatarisha maisha yake?

  5. Kwanini Roho Takatifu ilimwagwa kwa mitume?

  6. Kwanini Mitume walipewa uwezo kuzungumza lugha mbalimbali hadhalani?

  7. Kwanini Yesu Kristo alimpa Yohana Ufunuo?

  8. Je wale watakaofanywa wafalme na makuhani wakati Yesu arudipo watatawala wapi?

  9. Ni ipi Sala ya mwisho ya Yohana mwishni mwa Ufunuo ?

 

 

 

 

 

Swahili Title: 
MTUME PAULO AENEZA INJILI KATIKA ULIMWENGU WOTE WA KIRUMI
English files: 
Swahili Word file: