Exploring the Bible Course - 25

KUJA KWA UFALME

SOMO LA 25.

 

Katika masomo yote yalivyotangulia imeonyeshwa kuwa Mungu ataanzisha ufalme wake hapa duniani na kuwa yesu kristo atarudi toka Mbinguni kuja kuwa Mkuu wa Ufalme huo.

 • Katika siku za wafalme hawa Mungu wa mbinguni ataanzisha ufalme ambao hautavujwa na ufalme hautarithi shwa kwa watu wengine ila utavunjavunja na kumaliza kabisa falme hizi nyingine na utasimama milele “(Dan 2:44)

 • Na malaika wa saba akapiga tarumbeta yake: na kukawa na sauti kuu nyingimbinguni,zikisema,falme za Bwana wetu na za kristo wake na atazitawala milele na milele.”(ufunuo 11:15)

 • Na yesu alipokuwa amesema maneno haya wakati wangali wanaangalia alipaswa juu na wengi likampokea akatoweka machoni mwao na walipokuwa wa mikazia macho mbingu alipokuwa wa mekazia macho mbingu alipokuwa wa mekazia macho mbugumalipokuwa anakwenda juu tazama wanaume wawili walisimama karibu nao wakiwa wamevaa mavazi meupe ambao pia walisema nyie watu wamGalilaya kwa nini munasimama hapa mkikodolea Mbingu macho? Yesu huyu huyu ambaye ameondolewa kwenu na kupelekwa mbinguni atakuja kwa jinsi ile ile kama mlivyo mwona akienda mbinguni(matenndo 1:9-11)

 • Pia yesu alisimulia fumbo la mtuwa ukoo wa mfalme ambaye aliondoka kwenda nchi za mbali kujitafutia ufalme na halafu kwundi (luka 19:11-27)

Katika fumbo hili Yesu alionyesha kuwa angekuwenda Mbinguni kwa Baba yake alileini akawahakikishia kuwa angerudi kuanzisha ufalme wa Mungu duniani.

 

MATUKIO KUANZIA WAKATI HUO HADI KURUDI KWA YESU KRISTO.

Kwa kuzingatia maswala haya mapana sasa tuangalie mtiriliko wa mambo kama mulivyoelezwa katika Biblia,ambayo yatatokea tangu sasa hadi ufalme utakapoamrishwa duniani .Kadri tunavyokusunya marejesho haya tunapendezwa na mfululizo mzuri wa mambo kuhusu Mungu atakavyo ibadilisha dunia hii wakati kristo anaporudi na manufaa yatakayomfikia binadamu.

 

Uozo wa maadili kuendelea.

Uozo wa kimaadili uliopo duniani mtaendelea ambao haunabudi kuzaa ufisadi na ukatili matokeo yake yatafanana nay ale ya wakati wa Noah ina loti wakati dunia ilikuwa fisadi mbele ya Mungu na iliyojaa ukatili”(Mwanzo 6:11-13)likiwa toleo la mwanadamu kumwasiMungu.Hatima yake ilikuwa ni kuvunjika kwa ndoa na kusambalatika kwa maisha ya kifamilia wanaume na wanawake walijawa na tama mbaya za kila aina kufanya mamboyasiyostahili (mwanzo 6:2,5) Yesu mwenyewe alisema dunia itazama tena katika hali kama hiyo kabla ya kurudi kwake (luka 17:26-27) mathayo 24:36-39)

Uovu uliopotoka kabisa uliosababisha kuteketezwa kwa sodoma na Gomorrah utakuwa umeenea duniani wakati atakaporudi (luka 17:28-33).

Mpenzi wa njia ya Mungu kwa vyoovyote atahangaishwa na kuenea kwa ngono ya jinsia moja na kukubalika kwake,pamoja na picha za ngono na kuenzi uovu na ukatili uliomo katika jamii zetu leo.

 

WAKATI WA HOFU NA KIHORO.

Tatizo lingine litakalomkumba dunia kuelekea kurudi kwa yesu kristo ni hofu na hali ya kutojua mustakabali wa dunia yesu alipoulizwa na wafuasi wake kuhusu ishara zitakazoonekana kukaribia kurudi kwake alisema kuwa kutakuwa “mioyo ya wanaume italemewa na hofu na matazajio ya mambo yatakayokuja duniani” (Luka 21:26).

Ukatili na tishio la vitishio la ambavyo vimesababisha woga,mauti kuteseka na mharifu kwa watu wengi vilibashiriwa na Yesu.Hata hivyo Yesu aliendelea kusema “Na ndipo watakapomwona mwanawa Mwanadamu akija mawinguni akiwa na nguvu na utukufu Mkuu na mambo haya yatakapokuwa yameishatimia,tazameni juu,inueni vichwa vyenu,kwa kuwa uokovu wenu utakuwa umekaribia” (aya ya 27-28), Mmambo ya kutisha na woga amboa umeenea sasa sasa hivi ni ishara mojawapo ionyeshayo kwamba Yesu atarudi hivi kazibuni.

 

KUSHAMBULIWA KWA ISRAELI SIKU ZAJAZO.

MANABII.

Ezekieli na Danieli wote wawili walitabiri kuinukia kwa shukisho la kijeshi la nchi za kaskazini ambalo litawania Israeli na mashariki ya kati wakati ule ule ambapo jamii itakuwa katika hali hii ya uogo.Ezekieli katika sura yake ya 38 na Danieli katika sura ya 11:40-45 wanatoa muhtasari wa vita hii ya baadaye katika Israeli na mashariki ya kali .(wasomi wengi wanadokeza kuwa shirikisho hili la kaskazini litaongozwa na urusi ona somo la 16 na ramani kupata undani wa matukio haya)

Nabii zakaria katika sura 12 -14 pia aongoza habari zaidi kuhusu wamizi huu Shirikisho hili la kaskazini litakapojiungaza kijeshi katika mashariki ya kati ambazo “utavuta mataifa yote katika mzozo huu Israeli itakuwa imesimama imara kama taifa na Yerusalemu itakuwa chini ya udhubiti wa (Ezekieli 38:8,12,16) wayahudi.

Ukweli huu ambao kwanga huenda usionekane kama wa kutatamisha unadhikwisha matukio ambayo hayakuweza kutokea kabla ya 1948, kwa sababu taifa la Israeli lilianzishwa mwaka huo kwa mara ya kwanza katika miaka 2000 .

Tunaposoma zakaria 12 hadi 14 tunagundua yafuatayo:-

-Mungu ataifanya Israeli kitovu cha ugomvi (zakaria 12:1-3)

-Mataifa yote yatakusanyika kupigania kwa ajili ya Yerusalemu na mashariki 38:Danieli 11:40-45)

-Katika ugonvi huu wayahudi waishio Israeli wataumia sana (zakaria 12:1-2) na wengi watauliwa (zakaria 13:8,9-14,3)

-Hadi wakati huo Yesu kristo atakuwa amesharudi na kujionyesha mwenyewe binafsi kwa watu wa Israeli “watanitazama mimi waliyemtoboa “(zakaria 12:9-11) hunganisha na Yohana 19:37) ---Ya nini katika mikono yako?”naye atajibu :Haya ni majeraha niliyopata nikiwa katika nyumba ya rafiki zangu”zakaria 13:6)Mwishowe wataamini kutokana na ushahidi huu wa kushangaza kuwa kweli yeye ndiye masihi.

-Mungu atawezesha tetemeko kubwa kupasua kilima cha mizetuni.

Jambo hili litaziogopesha nguvu za kijeshi zilizokusanyika ndani ya Israeli na kusababisha kushindwa kwa nguvu hiyo.(zakalia 14:4-8,Ezekieli 38:18-22)

-Shirikisho la kaskazini litaharibiwa “kwenye mlima ya Israeli”(Ezekiel 39:1-6)

-Mungu kwa njia Yesu kristo atatangazwa kuwa mfalme –“Bwana atakuwa mfalme duniani kote”(zakasua 14:9)

-Yelusalemu itakuwa kitovu cha ibada cha ulimwengu wote na pia serikali yenye haki ambako wale wote watakaokuwa hai miongoni mwa mataif watakwenda kujifunza njia za Mungu na kumwabudu (Zakaria 14:16;Jeremia 3:17,Iasiah 2:2-4,micah 4:1-2)

 

ARMAGEDON - Hasira ya mungu juu ya mataifa.

Ujumbe wa manabii wa agano la kale ambao unazungumzia mataifayote kujikusanya ndani ya Israeli kwa nia ya kuwamia kijeshi yanapojitahidi kumtawala katika kitabu cha ufunuo mle ugomvi huo unaitwa “armagedon”na unapotikana katika ufunuo 16:14-16)mtume Yohana alionyesha matukio yatakayoishia katika kutekelezwa kwa nguvu hii ya kisiasa na kijeshi ambayo.itaivamia Israeli wakati wa kurudi kwa yesu kristo.Katika aya ya 14 Yohana aliona roho yenye wazimu (au mashetani ) yakienda kukusanya wafalme wa dunia ili waende “kwenye vita ya siku hiyo kuu ya Mungu mweza yote”. Mahala ambapo Mungu atakusanya mataifa hayo panaitwa Armageddon,katika higha ya kijahudi”(aya ya 16). Hapa Yohana anatupatia alama muhimu inayohusu maana ya neno “Armagegeddon”. Agano jipya limeandikwa katika lugha ya kigiriki lakini Yohana asema neno ni la “ kiyahudi” maana ya moja kwa moja ya neno hili ni “masuke yaliyomo katika bonde kwa ajili kupepetea kupungua au kuhukumu” Mungu alikusudia kukusanya mataifa kama mtu kama mtu anavyo kusanya katika mavuno ili kupura ili kuhukumu na kuonyesha uwezo wake mkubwa ua mamlaka katika enzi hizi zilizo mjari Mungu .

Nalezi Joeli alitumia lugha sawa hivyo alipo tabiri kusanyo la Mungu la watu wasio mjua Mungu (watu wa mataifa )kwaajili ya kuvuna na kupura kwa maana ya kuhukumu (Joel 3:9-17) Angalia mfuatano . Joel anazungumzia mataifa yanayo jivundikia siraha za vita. Harafu inakusanyika bondeni kwaajili ya mapambano, “bonde la johashapheti” (maana yake “hukumu ya Muangu) ambalo limefanikishwa kama bonde la kidron, mashariki mwa yerusaremu kati ya Yerusaremu na mlima wa mizeituni huko yanavunwa (katika bonde la maamuzi” (au kupura aya ya 14) hatima yake ni kuwa bwana Mungu wa islaeli atapaza sauti yake na “mbingu na dunia zitatetemeka” (aya ya 16). Anakuwa matumaini ya watu wake , Islaeli na nafanya maskani yake Yerusalemu kwanjia ya mwanae Bwana wetu yesu kristo (aya ya 17)kama Bwana wa mabwana na ufalme wa ufalme (ufunuo 17:14 ).

 

KURUDI KWA YESU KRISTO “TANZANIA NA KUJA KAMA MWIZI”

Katika Zakaria na katika ufunuo tunaambiwa mahsusi kwamba ni katika kilele cha mzozo huu mkubwa ndani ya Islaeli kati ya umoja wa kaskazini, Israel na mataifa yote mengine ndipo Yesu atakapo jionyesha kwa nguvu zidi ya mataifa (zakaria 12-13:6)Katika simurizi la ufunuo kuhusu “vita hii kuu ya Mungu Mweza yote”tunaona kuwa hapa onyo linatolewa “ Tanzama naja kama mwizi amebarikiwa yule akeshae na anaye vaa nguo zake asije akatembea uchi na watu kuona utupu wake” (ufunuo 16:14-16)kwa huyo wakati kujikusanya kwa mataifa katika mashariki ya kati kunaendelea watumishi waaminifu wa Yesu kristo wanambiwa kuwa huu ni wakati wa kutarajiwa kurudi kwa bwana wao wanao pewa onyo . akeshae kuhusu utayari wao binafsi wa tukio hili kuu na wanaambiwa “amebarikiwa yule akeshae” kuna haja ya sisi wote kutazamia kurudi kwake tukiwa tayari kumpokea fumbo la wanawake wenye busara na wale wapumbavu linafundisha vizuri kuwa baadhi ya ya wale waliojua kuwa bwana wao angekuja tena hawakuwa tayari baragumu rinalia. “Tazama bwana harusi aja nendeni mkampokee” (Mathayo 25:1:13) Somo alilo fundisha Yesu kutokana na fumbo hili lilikuwa “kwa hiyo kesheni kwasababu hamjui siku wala saa ambayo mwana wa Adamu atarudi “(aya ya 13

Yesu kristo ametuasa kutazamia kurudi kwake na kuwa mavazi ya haki, na nakuwa na matendo mema ili atakapoonekana tusiambulie kwakuwa waaminifu (ufunuo 16:15) Hatua ya kwanza katika maandalizi ya kukutana naye ni kuamini mafunzo ya biblia na kubatizwa kwa jina lake (marko 16:15-16; Matendo 8:12).

 

UFUNUO NA KUKUSANYA KATIKA KITI CHA HUKUMU CHA KRISTO.

Kutimizwa kwa ahadi zote kuu za agano la kale kunategemea kufuuka kwa waaini ili waweze kupokea tuzo zao kwa hiyo kutakuwa na kusanyiko la wazima na wafu walio fufuliwa watakaofufulishwa mbele ya yesu kristo ili wahukumiwe wakati wa kurudi kwake hapa duniani hili linarejewa katika sehemu nyingi za biashara Nukuu zifuatazo zinazungumzia mfufuo huu na hukumu.

-Nakuagiza wewe (Timoteo)mbele ya Mungu na Bwana wetu Yesu kristo ambaye atakuhukumu wazima a wafu, atakaporudi na ufalme wake. “(2 timoteo4:1)

 • Kutakuwa na wakati wa taarabu ambayo hayajawahi kutokea tangu liwepo taifa hadi wakati huo :na wakati huo ndipo watu wake watakapo kombolewa, wote watakaokutwa wameandikiwa katika kitabu. Nawengi wao ambao wamelala katika vumbi ya dunia wataamka baadhi kuamkia katika aibu na dharau ya milele . Nawatakao kuwa wamewaongoa wengi watang’ara kama nyota milele. “(Dani.12:1-3)

 • Danieli alitabili wakati wa ufufuo na kukusanyika kwenye hukumu. Alisema kwa ufufuo utatokea wakati huo (Dan.12:1), akia na maana ya “siku za mwisho ,” wakati wa taabu”kwa mataifa ya dunia mfufuo na hukumu vitafanyika kutakuwa na tunzo wakati wa hukumu wengine watapokea uzima wa milele na wataingia katika ufalme kumsaidia Yesu kristo kuweka msingi imara ya haki ya Mungu duniani hata hivyo wasioamini watafukuzwa kwa aibu kutoka machoni kwake wakafe tena milele. Kuonekana mbele ya kiti cha hukumu cha kristo kunalejewa katika nukuu zifuatazo

 • Sote tutasimama mbele ya kiti cha Kristo kila mmoja wetu atajieleza mbele ya Mungu (Warumi.14:10-12)

 • Kwa maana sote tutafufuka mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mmoja apokee mambo yaliyo fanyika ndani ya mwili wake kulingana nay ale alivyofanya yawe mema au mabaya!! (2 wakor.5:10)

 • Msiyaajabie haya :kwamaana saa yaja ambapo wote waliomo makabulini watasikia sauti yake nawatatoka waliofanya vizuri watafufuliwa na kuendelea na wale walio fanya vibaya watafufuliwa na kuhukumiwa kifo “ (Yh.5:28-29 )

Wengi walio lala wataamka “ ambao ndio “ wengi?

Mara nyingi swali litaulizwa “Je kila mtu aliye wahi kuish tangu Adamu na Eva ataamshwa kuhukumiwa?” Jibu fupi ni “ hapana” ni wale tu wanao wajibika kwa Mungu miongoni mwa waliokufa na walio hai ndio watakao chukuliwa kutoa maelezo mbele ya Yesu kristo wakati atakapo kuja tena. Yesu aliwaamuru wafuasi wake kwenda pote duniani na kufundisha injiri alisema : “ Enendeni kote duniani mkafundishe Injili kwakila kiumbe . Yeyote atakaye amini na kubatizwa ataokolewa lakini yule lakini yule asiye amini atahukumiwa” (marko. 16:15-16).hapa tunayo atabaka mawili ya walio wapowale wanao amini na kubatizwa. Hawa watasimama mbele ya kristo na kujieleza kuhusu huduma yao, na kama walikuwa waaminifu watapewa uzima wa milele Yesu alikuwa wazi katika baadhi ya mafudisho yake; kwa mfano mabikira watano wenye busara na mabikira watano wapumbavu (mathayo 25:1-13);Watumishi waaminifu na wele waovu (mathayo 25:14-30; mkilinganisha na ruka 19:11-27). Hapa twaona kwamba kutakuwa na mgawanyiko mbele ya kiti cha hukumu kati ya watumishi waaminifu katika huduma yao kwa Mungu. Walakini kuna kundi lingine la watu ambao wanawajibika kwa Mungu kwa kuwa walisikia na kuelewa injili lakini wakakataa kupokea ahadi ya Mungu ya uonnevu hawataamlishwa na kuhukumiwa na Yesu kwa kuamini . mfano wa kundi hili unaonekana katika Anania na Kayafa ambao wahusika na kuzungumza na Yesu kristo lakini wakamkana na kumkataa kuamini. Wataimlishwa ili waeleze sababu za kuto kuamini kwao na uovu Yesu atakapo rudi (Mathayo.26:64)

Nabado kuna kundi la watu ambao hawakuwahi kiusikia kweli wa neno la Mungu. Hili linajumuisha idadi kubwa ya watu. Wameishi maisha yao bila kumfahamu Mungu na mwanae Hawata fufuliwa kuhukumiwa kwa sababu Mungu hata adhibu wat kwasababu ya kuto mfahamu. Katika kundi hili twaambiwa “wamekufa, hawaishi,wamefariki, hawatafufuliwa ( Isaya26:14)halafu mtu ambaye anaheshimika lakini haelewi ni kama wanyama pori ambao hufa” (zaburi49:20)

Kuelewa somo la Biblia kuhusu nani atafika kwenye kiti cha hukumu tufanye kama ifuatavyo:

UZIMA WA MILELE NA TUZO YA WAAMINIFU.

Japo wengi wanaoamini kuwa wana roho isiyo kufa tumeona kuwa Biblia inaonyesha wazi kuwa binadamu I kiumbe kifacho na kikundi kwenye vumbi miongoni mwa wengi waliokufa wamo wale ambao wanasemekana kuwa “wamelala” kwa maana japo wamekufa wataamshwa na mwito wa Yesu Kristo arudipo katika wakorinto wa kwanza 15: Paulo alilinganisha ufu wa kawaida ambao kila mmoja wetu aliye toka kwa Adamu anao, nay ale matumaini ya ajabu kwa wale wote ambao wameishi ndani ya kristo kupitia ubatizo alisema katika Adamu wote wataishi wote tena atakapo rudi (aya ya22-23).

Paulo alieleza badiliko la hali ambalo wote watakao onekana kuwa waaminifu watapokea “Huyu mwenye kufa atakuwa amevaa kutokufa” kwamaana “kifo kimemezwa na ushindi “ (aya ya 51-56) Hivyo wale “ ambao kwa subira kutenda vizuri na kutenda kutafuta utukufu, heshima na kuto kufa watapewa uzima wa milele “ (Warumi 2:7)

 

KUTAWALA NA YESU

Watumishi wa Yesu kristo watafurahi kuhusishwa na katika kazi tukufu ya kuanzisha kuanzisha ufalme wa Mungu kwa maelekezo yake.Watatawala kama wafalme na wakuhani hapa duniani (ufunuo5:10)majukumu yao yatakuwa ya aina mbili kazi ya ufalme ni ktawala na katika utawala huu, akiwa na mamlaka ya kimungu. Kuhaniyako kati ya Mungu na Binadamu, akiwafundisha watu akiwafundisha watu sheria za za Mungu na kuwaonyesha namna ya kutengana na dhambi. Hivyo watakatifu watatawala kama wafalme katika kuimalisha sheria za na utulivu wa wa ufalme na kufanya kazi za kikuhani katika kuwafundishia watu wenyekua wa dunia njia za Mungu .

Mojawapo ya kaziza kwanza itakayo fanyika na watakatifu waamifu ni wakati huo, wasio kufa tena .

Wakiwa sawa na malaika (luka 20:36) ni kufuatana na Yesu kristo katika kudhibiti mataifa ambayo yatakaribishwa kusalimu amri kwa hiari au kulazimishwa (Zaburi 2,Zaburi 149:5-9: ufunuo Israeli itakusanyika tena.

Kama unavyoonekana katika zakaria 12 na 13 kutakuwa na mauaji ya kutisha ya wayahudi wasishio nchini mwao na ni kwa kuingiliwa kati kwa mauaji hayo na Yesu kristo tu ndiko kutakaowanusuru baadhi yao (13:8-9,14:1-3) kuokolewa kwao kwa ajabu na ushuhuda wa “Majeraha”yao mkononi mwa mkombozi wao (13:6) kutatosha kabisa kuwanyenyekeza (12:10-14) Halafu wakakiri kwa furaha kuwa Yesu ndiye masihi yule ambaye baba zao walimkana na kumtandika msalabani.

Halafu mwito utatolewa kwa wayahudi wengine wote waliotawanyika katika nchi mbali mbali dunia nzima kuja na kumshuhudia yesu kristo kama mfalme wao (Jeremia 30:10-11,Ezekiel 20:33-38)kukusanyika kwao tena Mungu anakufananisha na kutoka kwa wayahudi katika nchi ya misri chini ya Musa (Jeremia 16:14-15) wayahudi hawa pia watatakiwa kumkiri Yahweh kama Mungu wa Israeli na Yesu kristo Mwanawe kama Mkombozi wao mwishowe watakuwa wamefahamishwa kusudi la mungu kumtima Yesu kristo na pia watakuwa wamejifunga kuwa alikufa ili dhambi zao zisamehewe 1 petro 2:24; Isaya 53:4) watatakiwa kukubali kuwa “Agano hili jipya” lilidhihirishwa katika damu yake (Math 26:8-12) yeremiaah 31:31-34) waebrani 8:8-12) wale ambao hawatasalimu amri watahesabiwa kama waasi na “kufukuzwa”na hawataingia Israeli” tena (Ezekiel 20:38)

Wale ambao wataitikia wataunganishwa na wayahudi ambao tayari wanaishi Israel na kuwa taifa moja tena,Ezekieli anatoa picha ya Israel iliyoungana kwa maneno haya.

“Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mungu.Tanzania nitawachukua wana wa Israeli kutoka Miongoni mwa wapagani popote watakapokuwa na nitawakusanya kutoka kila upande na kuwaleta nchini mwao na nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi iliyoko kwenye milima ya Israeli na mfalme mmoja atakuwa mfalme wao wote na hawatakuwa mataifa mawili tena wala hawatakuwa wamegawanyika katika falme mbili tena (Ezekieli 37:21-22),ringanisha Yeremia 23:3-8)

 

Wito wa kuondokana na makosa na kukubali kweli ya Mungu.

Mojawapo ya changamoto za wazi kabisa na mabadiliko ambayo watu walio wengi dunia nzima watalazimika kukutana nayo ni kugundua kuwa dini yao imekuwa ya uongo mtupu.watafikia utambuzi wa kushangaza kwamba miongoni wao wa dini wamekuwa wakifundisha makosa na wamekuwa wakifuata imani za kishirikina zilizo buniwa na binadamu.

Kama wayahudi watakavyokuja kutambua kwamba uelewa wao kuhusu Biblia ilivyofundisha kuhusu masihi ulikuwa na makosa,hivyo hivyo mamilioni ya watu wataona kuwa wamekuwa wakifuata mafundisho ya uongo na ushirikina usiokuwa na manufaa si dini zisizokuwa za kikristo tu ambazo zitafahamishwa juu ya makosa ya Imani zao bali dini zilizonyingi za kikristo pia zitagundua kuwa zimekuwa zikifuata uongo na hekaya zinazofundishwa kwa jina makosa na hadithi zingefundishwa kwa jina la kristo na wengi wangewafuata wahimu hawa.

“kwa maana wakati utakuja ambao hawatastahimili mafundisho bora bali kwa tamaa zao wenyewe watajikusanyia walimu kwa ajili yao wenyewe ili makisio yao yafurahishwe,nao watageuza masikio yao kutoka kwenye kweli nao watageuzwa kando kufuata hadithi za uongo”(2 Tim.4-3-4)

“Miongoni mwenu kutakuwa na wakimu wa uongo ambao wataleta uzushi na hata lemukana Bwana aliyewaumba na hivyo kujiletea maangamizi ya haraka na wengi watafuata njia zao potofu ambao kwa sababu yao njia ya kweli itasemwa vibaya na kwa tamaa na kwa kutumia ulaghai watawatumia nyinyi kibiashara” (2 petro 2:2-3)

Historia vimeishadhihilisha tahiri hizi na makanisa mengi ya kikristo yanathibitisha usahihi wa tabiri hizi Imani ya kweli kama ilivyofundishwa na Yesu kristo na mitume ilifundishwa na Yesu kristo na mitume ilifundishwa kulingana na watu walivyotoka kujikusanyia maua mafundisho mapya yalianzishwa na watu kwa kutoweza kusoma Biblia wenyewe hawakuweza kuona makosa yaliyokuwa yanaingizwa kwenye mafundisho hayo mfumo wa kanisa ulianzishwa ukiwa na maaskofu na maaskofu wakuu na mwisho wake papa waprotestauti japo walikataa baadhi ya mambo yaliyopita kiasi ya kanisa katoliki na kujitenga nalo waliondoka na mafundisho makuu ya uongo ambayo kanisa lilikuwa linatumia.

Walakini mtume Yohana aliona siku ambayo Yesu kristo akisharudi hapa duniani tangazo litatolewa “Mwongopeni Mungu na mmpe utukufu utukufu kwa kuwa saa ya kuhukumu yake imefika ;na muwabudu yeye aliyeumba mbingu na dunia na bahari na chemchemi za maji (ufunuo 14;6-7)

Hapa watu watapewa nafasi ya kuachana na uongo na ushirikina waliokwisha fundishwa na kukiri kuwa Mungu amemtuma Yesu kristo kuja kuanzisha ufalme wake.Yohana aliona mapema kuwa kanisa la kikatiliko la Roma pamoja na makanisa mengine ya kikristo watatoa changamoto dhidi ya mamlaka ya kristo lakini yao hatazaa matunda yoyote kwa kuwa”mwanakondoo(Yesu kristo ) atayashinda kwa maana yeye ni Bwana wa mabwana na mfalme wa wafalme :na wale ambao wako pamoja naye wameitwa na wamechaguliwa na waaminifu”(ufunuo 17:14)

Mfumo wote wa kikatoliki pamoja na makanisa mengine yenye mafundisho yanayo karibiana na hayo ambayo yanaelezwa katika Bidha kihalali kama “Fumbo” Baby lon mkuu mama wa makahaba na machukizo ya dunia “ yatateketezwa kabisa (ufunuo 17:50 siku hiyo huu mfumo ulioasi utazungumziwa kama ile dola ya zamani yenye jina hilo hilo “Baby lon mkuu ameanguka ,ameanguka”na “hataonekana tena”(ufunuo 18:2-3,21) watu watangundua kuwa mfumo huu wa dini ambao umetawala maisha ya mamilioni ya watu kwa karibu miaka 2000 mlikuwa ni mfumo uliotengenezwa na mwanadamu wa haukuweza kuwapa wafuasi wake uokovu haukufuata njia za kristo hata kidogo na kwa kweli ni mada ya utabiri mwingi ambao kwao Mungu aliwatahadharisha watu dhidi yake.Onyo la kristo liko wazi.Tokeni ndani yake (yaani Babylon,au kanisa katoliki)watu wangu ili msiwe washiliki wa dhambi zake na ili msipokee mapigo yake kwa maana dhambi zake zimefika mbinguni na Mungu amekumbuka udhalimu wake”(ufunuo 18:4-5) kuwepo kwa dini za uongo –za kiyahudi kikristo na nyinginezo-zote zikifunuliwa kama za kimakosa njia sasa itakuwa wazi kwa uchumishaji wa dunia katika njia za Mungu na kweli Baada ya kupindua upinzani kisiasa,kijeshi na kidini kristo na watakatifu wake wasiokufa ataweza kuanza kazi kuu ya kufungua ufalme wa Mungu duniani.

 

Bwana atakuwa mfalme duniani kote.

Yerusalemu itakuwa mji mkuu wa ufalme na itatambuliwa hivyo na mataifa yote (Yerusalemu 3:17-18) itakuwa kitovu cha serikali yenye haki nay a kuelimisha katika “dunia ya Bwana “kwa kweli watu wa Mataifa yote watakwenda Yerusalemu mwaka hadi mwaka humwabudu mfalme Yesu kristo na kujifunza njia za Mungu “Na itatika katika siku za mwisho kuwa mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa juu yam lima na utakuwezwa juu ya vilima na mataifa yote yatamiminika kuelekea na watu wengi watakwenda na kusema njooni nyiye twende juu kwenye mlima wa Bwana kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo,naye atatufundisha njia zake nasi tutatembea katika njia vyake kwa kuwa katika sioni ndimo zitakapotoka sheria na neno la bwana litatoka Yerusalemu “(Isaya 2:2-4)

Na itatokea kwamba kila taifa litakalokuwa limeachwa kati ya mataifa yaliyopigana na Yerusalemu nalo litapanda kwenda yerusalemu mwaka hadi mwaka kuabudu mfalme,Bwana wa ukarimu na kufanya karamu ya taberna kulo”(Zakaria 14:16)

Mataifa yote yatakuwa chini ya utawala wa kristo (ufunuo 11:15) Israeli itakuwa walimu na mitume kumi na wawili (math19:28)

Kutakuwa na Hekalu “nyumba ya ibada kwa mataifa yote” itakayojengwa yerusalemu ambamo mataifa yote yatakuja kujifunza njia za Mungu na kumwabudu (Isaya 56:7) Mataifa yaliyo mengi yatakuja kwa furaha lakini yale yatakayokuyo kataa kwenda yataathirika kwa uasi wayo (zakaria 14:16-17) Habari za kwa kuhusu hekalu hili zimo katika sura za mwisho za utabili wa Ezekieli (40-48) kutokana na habari hizi tunaweza kupata picha vichwani mwetu ya jumla hili zuri ambamo Bwana mwetu Yesu Kristo atafanyia kazi yake.

Picha ya maneno ya Ufalme huu pamoja na mafao yatakayotolewa na mfalme kwa wanadamu wote inaonyeshwa katika zaburi 72 na mika 4: 1-5 kila mtu atahisi mara moja uzuri wa utawala wa kristo kuwa kazi ya kutawala kwa haki ni utulivu na uhakiki milele ( isaya 32: 1,17)

 

Utawala wa kristo wa miaka 1000.

Mtume Paulo asema kwamba Kristo atawala dunia hadi atakapowaweka adui wote chini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayeangamizwa ni kifo”. Vitu vyote vitakapokuwa chini ya kristo atamkabidhi Mungu ufalme wake “ ili Mungu awe yeye ni yeye.(1 Wakolinto 15:24-28) Hapo, kwa kweli dunia itakuwa imejaa utukufu wa Bwana” ( Hesabu 14:21) kipindi cha ufalme kimeelezwa kwetu katika kitabu cha Ufunuo. Humo tunaambiwa kuwa Kristo wa watakatifu wake wasiokufa watatawala kwa muda wa miaka 1000 ( ufunuo20: 4-6) baada ya miaka 6000 ya kuandaa watu kulipa jina lake heshima na utukufu, miaka mingine 1000 imetengwa katika mipango ya kimungu kwa ajili ya mfalme na watakatifu wake wasiokufa kujaza dunia kwa utukufu wa mungu. Katika milenia hii yote idadi yote ya watu wa dunia hii watapata fulsa ya kumtumikia mungu na Kristo mfalme kwa uaminifu na utii. Maelezo ya baadhi ya mabadiliko yatakayojiri pamoja na baraka zinazoandamana nayo, yamo katika sehemu mbalimabali za maandiko matakatifu ( Isaya 11: 4-9; 65:17-25; Amosi 9:11-15).

Kipindi hiki cha miaka 1000 ya utawala wa kristo kitaishia kwenye ufufuo wa pili na wa mwisho na kukusanya watu kwa ajili ya hukumu ya watu watakaokuwa wameishi wakati wa ufalme wa kristo. Tukio hili limeelezwa katika kitabu cha ufunuo 20:12 – 15.twaomba kuwa katika tamati ya hukumu hii “kifo na jehanam vilikuwa vimetupwa katika ziwa la moto” ( aya ya 14) kwa maana kwamba vitakuwa vimefagilwa mbali kutoka duniani milele. Halafu hatakuwa na kifo tena ( 1 Wakolinto 15:25-26) katika ufunuo 21:3 - 4 tunasoma juu ya wakati huu mzuri ajabu “Tazama Tebernaklo ya Mungu imo mongoni mwa watu na Mungu imo nao watakuwa watu wake na Mungu wao. Na Mungu atafutilia mbali machozi wala kilio na wala maumivu hayatakuwepo tena kwa kuwa mambo ya zamani yameshapita wakati huu kama Paulo alivyotabiri Mungu atakuwa amejikamilisha (Wakoro 15:28)Hivyo ufalme wa Mungu duniani ndiyo tatua ya mwisho ya kuelewa kwenye utimilifu wa kusudi tukufu ambalo Mungu alikuwa nalo tangu mwanzo kujaza dunia utukufu wake (hesabu 14:21) wale ambao ni wanae na mabantize wakisha jenga tabia kama yak wake kupita majaribu ya maisha watakuwa naye.Jumuia hii tukufu itakuwa imeungana na Baba na mwana kama Yesu mwenyewe alivyoomba mara kabla tu ya kutundikwa msalabani (Yoh,17:20-23)

 

Ufalme wako ufike”

Kutokana na somo la hapo juu tunapata uelewa wa ufalme mtukufu ambao Mungu ataanzisha duniani kulingana na ratiba iliyoonyeshwa Mungu atamtuma Yesu kristo hivi hii kubwa ya kuubadilisha ulimwengu akisadiwa na wafuasi wake waaminifu tukiwa na imani katika neno la Mungu na matumaini ambayo neno hilo linatupatia tunaweza kuingia kikamilifu katika maana halisi ya sala ambayo Yesu alifundisha wafuasi wake “(Mathayo 6:9-10) Tunapoissubili siku hii ambayo Mungu ameahidi ni upendeleo na jukumu letu kumwitikia kwa imani na utii.Mtume petro aliwatia moyo wafuasi wa Yesu siku hizo na vivyo hivyo sisi aliposema. “Fanyeni bidii ili kuchaguliwa na kutiwa kwenu kuwe kwa uhakika zaidi kuwa mlifanya hivyo hamtaanguka kwa kufanya hivyo lango la kuingia katika ufalme wa Bwana na mkombozi wetu Yesu kristo litawekwa wazi kwa ajili Yesu milele (2,petro 1:10-11)

 

MUHTASARI WA FUNDISHO

Yesu kristo atakuja tena duniani (Matendo 1:9-11)kusimika ufalme wa Mungu (dan 2:44;ufalme 11:15) katika fumbo la luka (19:11-27 Yesu kristo alitabili kuwa atapata mbinguni na kukaa kuumeni kwa Baba yake na baadaye kurudi duniani wakati ambao watumishi wake watahukumiwa na kupewa tuzo kabla ya kurudi kwake Yesu kristo dunia itaendelea kudidimia katika dhambi na uovu sawa na ufisadi na ukatili uliosababishwa hasira ya mungu wakati wa Mafuriko enzi za Noah (Mwanzo 6:1:13;angalia pia mathayo 24;36-39;Luka 17:26-27) na maangamizi ya sodoma (mwanzo 19 na pia luka 17:28-33)

Manabii wanatoa maelezo ya kina kuhusu shambulizi la Israeli na yerusalemu litakalofanywa na muungano wa mataifa ya kaskazini shambulizi hili litajiri wakati wayahudi watakapokuwa wamerudi katika nchi yao,Israeli na yerusalemu itakapokuwa mikononi mwao (Ezek 18:zakaria 12:14)kwenye kilele cha mapambano haya kati ya mataifa Yesu kristo atajionyesha akiwa na nguvu uweza wa mungu kuwafanya watu wote duniani wamtambuwe Mungu na kumkabili yeye mwenyewe kama masihi na Bwana (zakaria 12:9-11.13:6;14:4-9)

Armageddon ni neno la kiebrania ambalo linaeleza hukumu kuu ya Mungu ambayo itamiminwa juu ya mataifa yote wakati yesu anaporudi dunani ufunuo 16:14:16;Joeli 3:9-17)

Kurudi kwa Yesu kristo ni jambo ambalo litakuwa halitavajiwa kabisa isipokuwa na wale ambao watakuwa wamekesha kwa uaminifu na wamejiandaa kwa ajili ya siku hiyo kuu (ufunuo 16:15;mathayo 25:1-13)

Hatua ya kwanza katika maandalizi ya kumpokea Yesu kristo ni kuiamini injili na kubatizwa (marko 16:15-16)

Yesu atakaporudi atafufua watu ambao watatakiwa wahukumiwe na kukusanya wale wanaowajibika bado hai (timoteo 4:1) Danieli 12:1-3;Yohana 5:28-29)

Wale watakaokusanywa ili kuhukumiwa watajieleza kuhusu huduma yao kwa Mungu (warumi 14;12;2wakorinto 5:10) mafumbo mengi yanatoa picha ya kiti cha kurudi (mathayo 25:14-30;duka 19:11-270

Wale ambao hawatakuwa wamemjua Mungu na neno lake hawatahukumiwa kama watakuwa wamekufa hawatafufuliwa (isaya 26:14)

Wale watakaokuwa wamemtumikia Mungu na yesu kristo kwa uaminifu maisha yao yote watazawadiwa wa uzima wa milele(warumi 2:7;1 wakorintho 15:51-57)

Watumishi waaminifu wa Yesu kristo watamsaidia Yesu kuanzisha ufalme wa Mungu hapa duniani (ufunuo 5:10;20:6)

Yesu kristo watamsaidia Yesu kuanzisha ufalme wa Mungu hapa duniani (ufunuo 5:10;20:6)

Yesu kristo atajionyesha kwa wayahudi hai katika nchi ya Israeli atakaporudi (Zakaria 12:9-11;13;6) wayahudi waliotawanyika duniani kote watakusanywa ndani ya Israeli kushuhudia kuwa yesu yule yule amabye baba zao walimsuluhu ndiye mkombozi wao (ezekieli 37:21-22) Jeremia 23:3-8)

Mataifa yote yatatakiwa yambe yesu kristo heshima kama mfalme (zaburi 2:10-120 na kuitikia mwito wa kumwabudu na kumtumikia Mungu.

Mifumo iliyokufuru ya kikristo ikiongozwa na kanisa katoliki pamoja na dini zisizokuwa za kikristo ambazo zote zimedanganya mataifa kwa kufundisha mambo yasiyo ya kweli itafichuliwa na kutekelezwa (ufunuo 18:2-3;21;17:5)

Yesu kristo atatawala kama mfalme katika mji wa Yesrusalemu ambao utakuwa mji mkuu wa ufalme wa Mungu duniani (Yeremia 3:17;Isaya 2:2-4;zakaria 14;9,160

Hekalu litajengwa Yerusalemu ambamo mataifa yote yatakuja kumwabudu Mungu.litaitwa”Nyumba ya ibada ya mataifa yote”(Isaya 56:7 zakaliah 14:16-17)

Ufalme utasifika kwa haki na amani (zaburi 72:isaya 32;1,17)

Utawala wa Yesu kristo duniani utadumu miaka 100 (milenia) Ufunuo 20;2-5,1 wakoritho 15:22-28 baada ya hapo kutakuwa na ufufo wa wale walioishi na kufa katika kipindi hicho mwishoni mwa milenia hapatakuwa na kifo tena kwa kuwa watu wanao weza kufa hawatakuwepo tena duniani (Ufunuo 21:3-4)

Kusudi laMungu la kujaza dunia utukufu wake litakuwa limetumizwa (Hesabu 14:21)Mungu atakuwa kila kitu (! Wakor 15:280

 

MASWALI-SOMO LA 25,

 1. Orodhesha nukuu mbili za biblia zinazofundisha kuwa ufalme wa Mungu utaanzishwa duniani

 2. Tupe nukuu ya Biblia inayosema yesu kristo atarudi duniani

 3. Ni katika sehemu gani ya dunia ambayo mataifa yatakusanyika kwa ajili ya Armageddon?

 4. Ufunuo wa wafu utafanyika lini?

 5. Ni nani watakaofufuliwa kwa ajili ya hukumu ?

 6. Ni zawadi gani watakapopewa waaminifu /

 7. Ni nini kitakachotokea kwa wayahudi waliotawanyika pale Yesu atakaporudi?

 8. Mji mkuu wa ufalme utakuwa mji gani/

 9. Mataifa ya dunia yatajifunzaje njia za Mungu katika ufalme wa Mungu?

 10. Utawala wa kristo utadumu muda gani?

 11. Ni mimi kitakachotokea mwishoni mwa millennia?

 12. Maisha yatakuwa tofauti kwa jinsi baada ya millennia?

Swahili Title: 
KUJA KWA UFALME
English files: 
Swahili Word file: 
PDF file: