Exploring the Bible Course - 26

UANAFUNZI NDANI YA KRISTO LEO

 

SOMO LA 26

Tumekwisha ona kuwa ujumbe wa Injili ulio hubiliwa na mitume ulikuwa na dhamira au sehemu mbili (matendo 8: 12). Tayari tumeshaona “habari njema za ufalme wa Mungu”

Katika somo lililopita na sasa tutachunguza mambo yanayohusiana na “jina lake yesu kristo” nafsi yao katika maisha yetu ndani ya kristo.Maneno “Jina lake yesu kristo” kujumuisha kazi ya mungu kupitia mwanae katika kutoa msamaha wa dhambi kwa wanadamu anaye kufa, na zawadi ya kuishi milele yesu kristo akirudi hapa duniani. Mungu kupitia nabii Isaya, anasema yeye ni “Mungu mwenye haki, Mwokozi “Anaendelea” Niangalia mimi mkaokolewe enyi inchi zote za duniani mana mimi ni mungu hapana mwingine “(Isaya 45:21-22). Yesu mwenyewe alisema “kwa maana jinsi hii mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe nauzima wa milele, ulimwengu uokolewe katika yeye.”(Yohana 3:16-17), Petro aliwambia watawala wa Israeli kuwa:”Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilo pewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (matendo 4:12). Ni Kwa kuamini na kasha kubatizwa katika jina la bwana Yesu Kristo tu.tunaweza kuokolewa.Petro alipoulizwa katika sikukuu ya Pentekosti na wale wliokuwa wakimsiliza kwa makini “Tutendeje, ndugu zetu? (kwani walikuwa wamechomwa kwa ule ukatili walioufanya katika kumsulubisha mwana wa Mungu), alijibu,” Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi Zenu “(Matendo 2:37-38 , Petro baadaye akihubiri ujumbe wa wokovu kwa korneli mtawala wa kirumi,alielezea kwamba manabii wote wa Israeli walikuwa wameshuhudia “ ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo ladhambi”Korneli alikubali kwa Imani na kasha akabatizwa “kwa jina lake Yesu Kristo “(matendo10:43,48)

 

UBATIZO KATIKA KRISTO

Mtu anapobatizwa anajumuika pamoja na BwanaYesu, Kristo katika kifo, kuzikwa na ufufuo wake ( Warumi6:3-5).Tumeangalia tayari kwamba lazima kuwe na kukiri kwa dhambi iliyofanywa na toba ikionyeshwa katika kuacha mwenendo wa maisha ya nyuma, kabla ya mtu kubatizwa. Katika Warumi 6 Paulo anaeleza kwa maneno rahisi na ya kueleweka kuhusu umhimu wa ubatizo na matokeo yake juu ya mwanafunzi wa Kristo. Yesu, muda wote alikuwa mtiifu kwa mapenzi ya Baba yake.Utiifu huu mwishowe ulimchukua mpaka msalabani ambapo alisulubiwa kikatili na waovu. Ingawa “yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, Japo hakutenda dhambi, (waebrania4:15-16). Katika kifo chake alipa ushindi wa mwisho juu ya dhambi iliyomo ndani ya watoto wote wa Adamu na kusababisha wote, Isipokuwa yeye Yesu. Kwa msistizo kabisa tunaambiwa alikuwa na maumbile kama sisi tulivyo,”damu na mwili”-“yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo.” Hii ilikuwa muhimu, ili kwamba “kwa njia ya mauti amharibu yeye alikuwa na nguvu za mauti, yaani Ibilisi (diabolos), neno linaloendana uwezo Wa kutenda dhambi ambao wote tunaona –waebrania 2:14, Warumi 7:15-21, Angalia Somo la 24). Kwa sababu ya maisha yake yasiyona dhambi kwa utiifu wake,mpaka kifo cha msalabani,hai kuwezekana au haikuwa haki kwamba kaburi liendelee kumshikiria (matendo 2:23-24,’ Warumi6:9).Mungu,kwa haki Yake alimfufua kuja katika uhai tena na kumpa kutokuharibika katika uwepo wake(matendo2:32-36, Wafilipi2:8-10),Kwa sasa amekaa katika mkono wa kuume wa Mungu mbinguni,akiwa kuhani Mkuu akipatanisha kati ya Mungu na wale wanaomkaribia Mungu kupitia yeye (Waebrania7:25,2:17-8) Tumeshaona katika Warumi 6 kwamba katika ubatizo unatufanya tuungane pamoja na Yesu Kristo katika mauti yake na ufufuko wake. Kwanza hebu tuangalie jinsi tunavyohusiana na kifo chake

Paulo anasema: “tukijua neno hili,ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye,ili mwili wa dhambi ubatilike,tusitumikie dhambi tena kwa kuwa yeye aliye kufa amesabiwa haki mbali na dhambi “(warumi6:6-7). Hivyo katika ubatizo tunaonyesha tamaa yetu kuungana na mauti ya Bwana wetu, mauti ambayo kwayo alimwangamiza, mara moja ndani yake mwenyewe yule diabolos, yale maumbile ya dhambi ambayo yapo kwetu sisi sote. Paulo anaita “utu wa kale” katika ubatizo “utu wetu wa kale.Ulisulubishwa pamoja naye’ yaanitukizikana njia za dhambi ambazo zimetutawala maisha yetu, kwa kukiri kwamba sisi tu watenda dhambi tukihitaji kutubu.Tunakiri kwamba tunapaswa kufa kutokana na dhambi zetu, kwani tumejifunza kwamba ‘’mshahara wa dhambi ni mauti ’’[warumi 6 ; 23). Tunapotoka nje ya maji ya ubatizo,Paulo anaelezea usambamba wake-n sawasawa na ufunuo wa Yesu.Tunakuja tena kwnye njia mpya ya maisha, tukimtumikia Mungu akiwa kama Bwana wetu mpya. Paulo anatufafanulia suala hili kwa namna hii. Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima (Warumi 6; 4).

Ni katika’’Upya waUzima ‘ ambao mwanafunzi anafanya juhudi katika kumfuata kristo. Katika njia ya uzima ambayo kristo anaonekana akiishi ndani yetu tunapofanya juhudi yakufuata mfano wake (1petro 2;21-25) .Paulo,kwa kufikiri kiundani anaelezea juu ya mabadiliko ambayo yalitokea katika maisha yake; Nimesulubiwa pamoja na kristo lakini ni hai .Wala si mimi, tena ,bali kristo yu hai ndani yangu, na uhai ni lionao sasa katika mwili, ninao katika imani ya mwana wa Mungu, ambaye alimpenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu (Wagalatia 2;20).

Ni kwa upendo wa kristo, uliofunuliwa katika mapenzi yake ya kuutoa uhai wake kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, ambazo zilimfanya Paulo kukubali kujikabidhi maisha yake katika huduma ya Bwana wake [2Wakorintho 5; 14, 15 1Yohana 3; 16). Yesu alikuwa anasema. ‘Hakuna aliye kuwa na upendomwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mwaamuruyo’’ (Yohana 15; 13-14) Wale ambao, kama Paulo, wana ujuzi sahihi wa jinsi kristo amewakomboa kutoka katika dhambi na kifo, watataka kusulubisha ‘utu wakale’na kufufuka katika ‘ Upya wa Uzima ‘Ndani ya kristo kwa kuzifuata amri zake. Ni Kwa kuenenda kutokana na amri hizi ambapo kristo anaonekana ‘ndani yetu ni kwakupitia mafundisho yake ambapo tabia yetu mpya itaimarika (Wakolosai 3:1-14; Wagalatia 5:19-26, Waefeso 4:17-32; 5:1-21). Zingatia: muhutasair wa amri za kristo umeandikwa kwenye hitimisho la somo hili;

KUENENDA KATIKA ‘UPYA WA UZIMA’

Paulo anasema kwamba katika hali yetu mpya tuna badiliko la Bwana na la huduma na huduma. Ambapo hapo mwanzoni muumini aliitumikia ‘dhambi’ Na kuridhisha tamaa zake, sasa,kupitia ubatizo, amekuwa huru kutoka katika utumwa wa dhambi na kuitumikia”haki “(Warumi 6; 17-18).Paulo anaielezea huduma hii mpya ya “kutakaswa,na mwishowe, Uzima wa milele;”Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru,na kuwambali na dhambi,nakufanywa watumwa wa mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele .Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti,’Bali karama ya mungu ni uzima wa milele katika kristo Yesu Bwana wetu”(Warumi 6:22-23). Tena badiliko linazungumzwa kama hivi:”Mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza ya utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kuda nganya,na ‘mkavae utu mpya’ulioumbwa kwa namna ya mungu katika haki na utakatifu wa kweli (Waefeso 4: 22-24)” utu mpya “ Unaonekana katika namna mpya ya kufikiri na kutenda, sawa sawa na Bwana Yesu kristo.Maisha ya mwanafunzi ya talenga juu ya kupenda huduma ya Mungu kwa juhudi kutokana na neema Yake katika kumtoa Yesu kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi (Tito 2: 11-14).Atapenda kuonyesha tabia nzuri katika maisha yake inayotokana na mungu kama ilivyofunuliwa katika Biblia.(Kutoka 34:6, 7) Vilevile ataona kwamba, hapendezewi njia potofu na za uovu wa Dunia hii. Kama Yesu kristo, atapenda haki na kuchukia uovu (Zaburi 45:7, Waebrania 1:9) Hivyo Paulo anamalizia kwa kusema: “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya kristo amekuwa kiumbe kipya, ya kale ya mepita, tazama! yamekuwa mapya (2Wakoritho 5:17)

UTU MPYA ULIOZALIWA KUTOKANA N A NENO LA MUNGU

Huu “Utu mpya” Paulo anasema “unaofanywa upya upate ufahamu sawa sawa na mfano wake yeye aliye umba” (Wakolosai 3:10). Utu mpya unajitokeza kwa sababu ya njia mpya ya ujuzi sahihi ya Injili. Badiliko hilo limetokana na usomaji wa makini na kufuata neno la mungu.Yakobo anasema kwamba mungu amezaa watoto wake kupitia “neno la kweli” (Yakobo 1:18). Petro anasema kwamba wale wanaokubali kwa imani na utii kwenye Injili kuwa “mmezaliwa mara ya pili, Si kwa mbegu ihalibikayo, bali ile isiyo haribika, kwa neno la mungu lenye uzima lidumulo milele. Maana mwili wote ni lililohubiriwa kama ma jani, Na fahari yake yote kama ua la majani.. Majani hukauka na ua lake huanguka, Bali neno la Bwana huduma hata milele .Na neno hilo ni neno lile jema kwenu” ( 1Petro 1: 23- 25, CP Isaya 40: 6-8 ambayo kwao Petro ananukuu).

Maumbile ya mwanadamu, ni kwamba, atapotea endapo kama mwanadamu ameruhusu neno la uzima wa Mungu kuweza kuka moyoni mwake na kubadili maisha yake Mungu atampa mtu huyo uzima wa milele. Yesu pia alikuwa ameshatoa utofauti kati ya njia mbili, moja iongozayo uzimani na nyingine kifoni aliposema:”Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai, Maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena uzima.”(Yohana 6: 63)

USOMAJI-BIBLIA KILA SIKU.

Bwana Yesu kristo anatuvuta umakini kwenye hili somo muhimu sana anapo nukuu (kumbukumbu la Tolati 8:3). ”Mtu hataishi kwa mkate tu,ilakwa kila neno litokalo katika kinywa cha mungu .” Usomaji wa kila siku wa Biblia ni muhimu kwa mwanafunzi wa kristo kama mkate wake wa kila siku.kwa sababu mwanafunzi amezaliwa kwa kupitia neno la mungu, hivyo ni hekima yake kuboresha maisha ya kiroho kutoka kwenye neno hilo kila siku ili kuhakikisha ukuaji imara na wenye afya kiroho. Hii ndivyo kristo anapaswa kuonekana akiishi ndani yake. Daudi anazungumzia baraka ya mtu ambaye, anaelekea kutoka katika kundi la waovu, kufurahia mwenyewe” Sheria Bwana” na” Sheria yake huitafakari mchana na usiku” ( Zaburi 1).

Ni kwa kupitia usomaji binafsi Biblia ambao utamwezesha mwanafunzi kuimarishwa katika” Utu wa ndani” (Warumi 7: 22).Atajisikia anahitaji pia kujumuika na wengine ambao pia hua mini Injili hiyo hiyo ya kweli na kufarijika kwa furaha ya pamoja ambayo hutokana na kushiriki tumaini moja katika kristo. Mungu hupenda kuona watoto wake wakifurahia kuzungumza miongoni mwao wenyewe kuhusu neno lake na njia zake, kama na bii malaki anayo tuambia . Ndipo wale waliomcha BWANA watakuwa wana semezana wao. Nao watakuwa wangu, asema BWANA wa majeshi, katika siku ile ni fanyayo, naam, watakuwa hazina yangu hasa, nami nitawaachia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe amtumikiaye” ( Malaki 3:16-17).

KUDUMU KATIKA MAOMBI

Moja ya upendeleo mkuu ambao mwanafunzi mpya aliyebatizwa sasa anao ni kumkaribia Mungu kwa maombi kupitia Bwana Yesu kristo ambaye, akiwa upande wa kuume wa Mungu ,hufanya kazi ya upatanisho kama kuhani Mkuu kwa niaba yake ilikusamehe dhambi zake ( warumi 8:34 , Waebrania 7:25).

Hata hivyo ingawa bila ubatizo katika kristo hakuna ondolea la dhambi ni muhimu kukumbuka kwamba Mungu husikia maombi ya wale wanaotafuta kujua na kuelewa njia zake na kumtukia yeye. Tuna mfano wa Korineli ambaye alikuwa akimuomba Mungu mara kwa mara na hata hivyo Petro alitumwa ilikumuonyesha njia ya wokovu kupitia yesu Kristo (Matendo 10:1-6).Vilevile tunasoma kuhusu Lidia na nyumba yake ambao walikuwa watu wa maombi na Mungu alimtuma Paulo kwenda Filipi ilikuwa kwamba waisikie kweli ya Injili (matendo16:13).Wote kati ya Korineli na Lidia na nyumba zao walibatizwa baada ya kuisikia Injili (matendo10:48 16:14-15).

Mwanafunzi anaweza kujifunza kukua katika maombi kwa kutafakari baadhi ya maombi yaliyo andikwa katika Biblia.maombi ya wanaume na wanawake waaminifu yanafunza kubw. Tunaweza tukaona mahitaji yetu yakiwa sawa kamailivyo katika maombi yao. Wengi wamepata nguvu na faraja kutokana na maombi kama Zaburi 23. Mtume Paulo mara kwa mara alikuwa akiyaombea makundi ya waumini aliowajua.mfano wa hili umeandikwa katika (Wakolosai 1:9-14), ambayo hufaa kwa kujifunza kwani inatusaidia sisi kuona jinsi ya kuwaombea wengine.Wanafunzi wa.

Yesu waliwahi kumuomba siku moja awafundishe jinsi ya kusali. Matokeo yake ilikuwa ni sala ya ajabu ambayo kwa ukawaida huitwa “Sala ya Bwana” ambayo hutupatia kielelezo cha kufuata katika maombi yetu (Luka11:1-4’ na sala kiundani zaidi iliyo katika (Mathayo 6:7-15). Hata hivyo, Yesu alionya juu ya kurudia rudia maombi ambapo akili na moyohavihusiki. Alisema.nanyi mkiwa. Katika kusali, msipayuke- payuke, kama watu wamataifa, maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. .Basi msifanane na hao, maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba” (Mathayo 6:7-8).

Siyo tu mwanafunzi wa Kristo atamkaribia Mungu kumsifu na kutafuta mwongozo wa kila siku na uangalizi ,bali atatoa shukrani zake kwake kwa ajili ya baraka nyingi anazozipata. Yesu anatupatia mfano wa kutoa shukrani kwa ajili ya chakula kabla ya kula alipolisha makutano. Akaitwaa ile mikate saba na vile vya samaki vichache akashukuru akavimega akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano”(15:36, nao pia Yohana 6:11, matendo27:35, 1 Timotheo 4:3-4). Kuna mida ambayo mwanafunzi.atatoa maombi kuomba msaada kwa ajili yake mwenyewe au kwa ajili ya wengine katika vipindi vya shida, lakini pia anapaswa kukumbuka kuwa kuomba tu kutokana na mapenzi ya Mungu. Mungu hujua kile kilicho bora zaidi kwetu kuliko tunavyotaka, na anaweza asitupatue mahitaji yetu siku Zote. Ni katika hali hii atafuata maelekezo ya Paulo: “bali katika kila neno kwa kusali nakuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu (Wafilipi 4:6). Kwa kuona mahitaji na faida ya maombi mtu atadumu sana katika kuomba na faida ya maombi (Wakolosai 4:2)

KUTAFUTA MSAMAHA WA DHAMBI

Mwanafunzi, akishabatizwa tayari na akionyesha juhudi ya kumtumikia Mungu na kuacha njia yake kimawazo na kitabia mara kundua kwamba tamaa yake ya kumtaka Mungu tena ili aokolewe kutokana dhambi. Hofu ya kweli husukumwa juu yake akiwa bado ana maumbile yaleyale ya mwili na damu pamoja na udhaifu wake na tamaa mbaya. Dhambi zake za nyuma zilishasamehewa alipobatizwa, lakini masikini ametenda dhambi tena .Mtume Paulo kama wanafunzi wote wa Bwana, alitishwa na ukweli huu.Alikataa kwamba ingawa tamaa yake ilikuwa ni kumtumikia Bwana kwa juhudi zote, dhambi ilimdanganya na akaanguka chini warumi (7:18-24). Bado Paulo alijua kutokana na hali hii si kwamba hakuna jinsi alifurahia katika paji upya wa Mungu wa Mwokozi na mpatanishi, namshukuru Mungu kwa Yesu kristo Bwana wetu (mstari 25). Kuna faraja ilioje katika kujua kwamba tunaye mwombezi kwa Baba, Yesu kristo mwenye haki (1Yohana 2:1-2) na tukiziungama dhambi zetu yeye ni mwaminifu na hata atatuondolea dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote(1Yohana1:9). Hivyo mwanfunzi ataelewa uhitaji wetu wa kila siku wa musamaha ikli apate kibali mbele za Mungu. Hii ni sehemu ya Kielelezo ambayo Bwana aliwafundisha wanafunzi wake (Mathayo 6:12) kama Mfalme Daudi ataomba hii kwamba Mungu amuongoze katika njia za haki kwa ajili ya jina lake (Zaburi 23,3 Mathayo 6:13)

 

 

KUKUSANYIKA PAMOJA ILI KUMKUMBUKA KRISTO.

Desturi ya wanafunzi wa mwanzo ilikuwa ni kukusanyika siku ya kwanza ya juma ili kumkumbuka Bwana Yesu Kristo kama alivyowaamuru (Matendo 20:7). Pamoja na kwamba siku ya kwanza ya juma hubaki kuwa ni muda mzuri kwa wengi leo kukutana, siku, muda au sehemu si ya muhimu.

 

Yesu alikuwa amewaamuru waafunzi wake kumkumbuka mara kwa mara kwa ukawaida katika sherehe rahisi tu aliyoianzisha – katika kumega mkatena kunywa divai. Mkate ulitakiwa kuwakilisha mwili wake na divai ilitakiwa kuwakumbusha kuhusu damu iliyomwagika (Mathayo 26:26-29, Luka 22:19-20). Mtume Paulo aliuzungumzia huu ukumbusho wa Bwana katika barua yake kwa wanafunzi wa korintho akisisitiza utoaji au umuhimu mkubwa juu ya kile walichokuwa wanafanya (1Kirintho 11:23-29, 10: 16-17). Pia aliwakumbusha kuwa walipo kusanyika, wanawake lazima wafunike vichwa vyao (1 korintho 11:4-5, 13) na kwamba jukumu la kuzungumza na kufundisha katika makutaniko ni la wanaume (1 korintho 14:34, 1Timothy2:12). Wanafunzi leo hufuata agizo hili la Bwana wao na kukutana pamoja kila juma ili kumwabudu Mungu na kumkumbuka mwanaye katika njia iliyoagizwa.

 

Hata hivyo endapo muamini yuko mbali na wengine ambao wana imani na tumaini moja bado anapaswa kumkumbuka Bwana kwa ukawaida kama alivyoamuru. Kuna uhitaji wa kutenga muda wa kuomba, kusoma neno la Mungu na kushiriki mkate na divai, akikumbuka tendo la ajabu la dhabihu ya Bwana ambalo kwalo dhambi zake zimesamehewa. Japo yupo peke yake, ni sehemu ya familia ya Mungu duniani pote, na anaweza kufanyika kutokana na ukweli kwamba wengi kokote kule duniani walikuwa wafanya vinyo hiyo wakimuabudi Mungu na kumukumbuka mwanaye.

 

Ni vyema kukumbuka kujua kujua kuwa wale ambao huumega mkate katika njia hii hufanya hivyo kutokana na msingi walionao wa uelewa wa ukweli wa Bibilia.

Baada ya kubatizwa kwa wanafunzi wakawa wakidumu katika fundisho la Mitume na katika ushirika na katika kuumega mkate, katika kusali(Matendo 2:42 ) Ushirika katika maana ya kuungama pamoja na Mungu katika Kristo huwezekana tu kwa wale ambao huamini mambo yaliyofunuliwa katikaneno la Mungu ..Mitume walifundisha kwa mba mwenendo wao hauendani na Injili au ambao hufundisha mambo ambayo si fundisho lakweli, hawatakiwi katika ushirika {I wakorintho 5: 4-5, Itimotheo 1; 16-19, Tito 3; 10; 2 Yohana 10-1I). Hivyo, kamawaumini haujabatizwa katika Ukweli kama ilivyo katika Yesu hatuko huru kuimega mkate pamoja na wale walio katika makamoa . Mengine au wale wanaofuata mafundisho ya sio sahihi.

 

Wanafunzi katika karne ya kwanza pia walikutana pamoja kwa jili ya maombi na kujadili juu ya neno la Mungu . Mwanzoni Agano la kale lilikuwa ndio msingi wa mafunzo na mjada la, Lakini Injili na Nyaraka zilipoandikwa na Mitume tayari,hizipia zilisomwa {Wakolosai 4; 16) Kulikuwa na Umakini karika kujifunza na kufikiri juu ya neno la mungu ili waweze kuwana fahamu zaidi kuhusu njia zake na kumkalibia zaidi. Wale ambao hawakuendelea kudumu katika kupita ujuzi zaidi nen la mungu walikanywa (Waebrania 5:12-14, 1 Petro 2:1-2 )

 

Mitume walielewa kuwa imani ingeimanishwa tu kwa kuendelea kusoma neno la mungu ( Waebrania 10:17 ). Uchaji wa mtu pia ungekuwa tu kwa kufuatilia na kufikili tabia ya mungu kama alivyojidhihirisha katika kujushughulisha kwake kwa wanaume na wanawake hapo nyuma na kwakuona tabia hiyo ilivyo jidhihilisha kwa umakini katika maisha ya Bwana yesu kristo.

Wanafunzi wa Bwana leo bado wanafurahi kukutana pamoja kujadili Biblia na kusisitiza mmoja kwa mwenzake kuzifuata nyayo za Bwana yesu kristo ( 1 Petro 2:21-24, 2 Timotheo 3:16-17, 2 Petro 1:19-21, Waebrania 10:24-25 )

 

KRISTO – KICHWA CHA KANISA

Kielelezo kwa ajili ya maisha ya mtu binafsi katika Kristo na maisha ya miongoni mwa wanafunzi kimewekwa kwa ajili yetu katika mwongozo wa mtume unapopatikana katika Agano Jipya. Kama jumuiya za waumini zilivyoimarishwa kipindi cha ulimwengu wa kidini mitume waliendelea kuwakumbusha kwamba wote walikuwa ni sehemu ya ule “mwili mmoja” ambao kwao Yesu Kristo alikuwa “kichwa” (Waefeso 1:22-23, Wakolosai 1:18, 2:19). Jumuiya hizi mbalimbali ziliitwa “eklezia” likimaanishwa walioitwa na tumeshaelezea kuhusu maana ya neno hili katika somo la 23. waumini wa eklezia lazima wasisahau ukweli kwamba wao ni watu tenge “walioitwa” kumutukuza mungu katika maisha yao. Ingawa jumuiya zote za waumin iziliunganishika kwa “Imani moja” na “tumaini moja” katika Kristo hata hivyo kila jumuiya ilijiendesha katika shughuli zake za ndani. Sifa za wale ambao walitakiwa kuchafuliwa kwa ajili ya uangalizi na mwongozo wa hazi eklezea limetolewa kwa undani katika 1 Timotheo 3:1-7, Tito 1:5-9.

 

Kwasababu Yesu kristo alikuwa ndiye “kichwa” cha “mwili mmoja” aliyekubaliwa kwa ajili ya waumini (Waefeso 122-23, 4:15-16), ilieleweka kwamba kila jumuiya iliwajibika kwake. itakuwa na mlolongo wa uongozi uliwafanywa na mitume kama vile bodi kuu Papa, Baba, Askofu mkuu au nabii. Wale waliotoka katika mafundisho ya ukweli ya mitume waliokuwa ni wale ambao, kwa uchoyo wao waliwanyonya wafuasi wao, kama vile mtume Petro alivyotanguliya kuwaonya eklezia za mwanzo ambazo kwanzo aliandika (2 Petro 2:1-3). Inaeleweka wazi kwa zaidi ya mamia ya miaka kwamba uchoyo wa viongozi wa makanisa umegeuza dini kuwa mfumo wa kupatia pesa. Wale wanaojua unabii wa Petro wanaelewa namna gani mifumo ya makanisa ilivyofuata hili yakitimiza unabii wake wa suala hili. Aliwaonya kuwa walimu wa uongo wangeinuka na kujipatia “faida kwenu” ( 2 Petro 2:3 )

 

KIFUNGO KIMOJA CHA IMANI NA UPENDO.

Ingawa kila eklezia au kundi la waumini waliendesha mambo yao wenyewe kulikuwa na kifungo cha umoja ambacho kiliunganisha jumuiya popote duniani waliungana kwa sababu walishiliki imani moja tumaini moja na upendo wa Mungu, wa Yesu Kristo mwanaye, na wakila mmoja. Paulo aliwasisitiza waumini ila mmoja kuwa waaminifu katika yeye aliyekuwa amewaita, “kujitahidi kuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani kwani aliwakumbusha kuwa walikuwa “mwili mmoja na tumaini moja …. Imani moja (Waefeso 4:1-7)

 

Kifungu hicho kilichowaunganisha ndugu wa Bwana ni cha ajabu kilisoma katika nyaraka kwenye Agano Jipya. Kulikuwa na uangalizi kati ya makanisa hata kwa wale ambao wasingeweza kukutana uso kwa uso na ukarimu kwa wale waliosafiri. Kila muumini alikubalika na kutunzwa kwa upendo kwa ajili ya ustawi wake (Yohana 13:34-35, Waefeso 4:16, Wakolosai 3:12-17). Walielewa sana kwamba wote walikuwa ni wana wa Baba wa Mbinguni, waliozaliwa kwa neema yake na hiki ndicho kilichowalazimu kuwa na upendo wa kindugu ambao ungeonekana katika familia ya Mungu. Ukweli waliitana “ndugu’ na “dada”kama kikumbusha cha hadhi ambayo kila mmoja anayo na kufurahia katika Kristo (2Petro 3:15, Warumi 16:1, Wakolosai 1:2).

 

Upendo huu ulikuwepo katika makanisa hayo wakati huo na unaoonekana miongoni mwa wanafunzi leo unaelezwa vyema na mtume Yohana: ‘Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma mwanaye kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi imetupasa na sisis kupendana (1Yohana 4:10-11)

 

NAFASI YA MWANAFUNZI KATIKA JAMII

Mmoja ya sifa za mwanafunzi wa Bwana katika karne ya kwanza ilkuwa ni kujitenga kabisa kutoka katika shughuli za kisiasa na kijamii katika jamii wanamoishi. Ingawa Paulo anaelezewa kuwa akiwa ameshaupindua ulimwengu wakirumi wa kipagani (matendo 17:6) alifanya hili kupitia kuhubiri kwake Injili. Wanafunzi walijiona wenyewe kama Abrahamu, “wageni na wasafiri juu ya nchi” (Waebrania 11:13) na walijilinda wenyewe kutoka katika shughuliza kisiasa. Nguvu ya kazi yao ipo kwenye ujumbe waliouchukuwa na maisha ambayo waliishi.

 

Ujumbe huo ulifunua kusudi la kimungu kwa dunia. Ulionyesha kutokuweza kwa juhudi za mwanadamu katika kutatua matatizo ulimwengu na ulionyesha wazi uovu wa jamii ile walimo kuwa wakiishi. Hawakujiingiza katika shughuli za siasa au jeshi, wakiamini nakuelewa kwamba ilkuwa vibaya kwa wafuasi Mungu kufanya hivyo.

 

Amri za Kristo zinaeleweka sana. Wale wanaomfuata kristo hawapaswi kufanya uvunjifu au kuwadhuru wengine. Yesu alifundisha: “mmesikia kwamba imenenwa, jicho kwa jicho, na jino kwa jino, lakini mimi nawaambia, msishindane namtu mwovu, lakini akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie najoho pia” na pia “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na umchukie adui yako, lakini mimi nawaambia wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi” [Mathayo 5:38-44]. Baadaye, kundi la watu, walipokuja kumkamata Yesu na Petro alipotumia panga lake kumlinda Bwana wake, Yesu alisema, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga wataangamia kwa upanga” [Mathayo 26:52]

 

Wanafunzi walijua kwamba tumaini pekee kwa ulimwengu lilikuwa ni kurudi kwa Yesu Kristo na Ufalme wa Mungu ambao angeumalisha [Mathayo 5:39-44, 26:52, Daudi 4:17]. Kwa hiyo walifuata mafundisho ya Paulo na hawakujiingiza katika mambo ya ulimwengu. Walifuata fundisho la Paulo, “Tokeni kati yao, mkatengwe nao” ili kwamba wajitumee kutoka katika uchafu wa ulimwengu usio namaadili hivyo kutimiza “Utakatifu katia kumcha Mungu” [2Wakorintho 6:14-7:1]

 

Ingawa Paulo na mitume wengine waliwafundisha wanafunzi kutokujiingiza katika mambo ya kisiasa katika jamii, Walipaswa kwa kupenda kwao wanyenyekee kwa viongozi na kutii sheria ya nchi ambapo kwa kufanya hivyo havipingani na dhamira zao mbele za Mungu. Waliwasisitiza waombe kwa ajili ya mwongozo wa pekee wa Mungu juu ya walio kwenye mamlaka ili kwamba watunge sheria ambazo zingewapa uhuru wa kuabudu [Timotheo 2:1-6, Warumi 13:1-10, 1Petro 2:11-25].

 

Mwanafunzi leo watafuata mfano wao wa kujitenga kutokana na kujihusisha katika shughuli za kisiasa za ulimwengu huu, akisubiri kurudi kwa Yesu Kristo na kuimarishwa kwa ufalme wa Mungu .Kama Paulo ataona kwamba uenyeji wake ni kwenye ufalme ujao .”Kwa maana sisi wenyeji wetu uko Mbinguni, kutoka huko tena tunamtazama Mwokozi, Bwana Yesu Kristo” (Wafilipi3:20)

 

KUHUBIRI “HABARI NJEMA

Utakumbuka kwamba neno Injili humaanisha “habari njema”au kuhubiri habari njema”. Ujumbe wa wokovu kutoka katika dhambi na kifo na kuja kwa ufalme utakaoimarishwa hapa duniani ni kweli ni “habari njema”. Yesu aliwambiawanafunzi “Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri injili au habari njema kwa kila kiumbe. Aaminiaye na kubatizwa ataokoka”(Marko 16:15-16). Baada ya mtu kusikia na kuelewa hii “habari njema “ na kuiamini na kuitii kwa kubatizwa ,alifurahia mahusiano mapya ambayo sasa awayo pamoja na Mungu na Kristo. Hivyo kulikuwa na tamaa kubwa sana ya kushiriki hii “habari njema”na wengine ili kwamba nao pia waweze kushiriki tumaini la Injili.

 

Hii ndiyo jinsi ukristo ulivyoenea kiu rahisi katika utawala wote wa kirumi –warumi wa lipoongezeka waliwaambia wengine “habari njema”au Injili. Paulo kwa mfano, anawaambia waumini wa Thesalonike jinsi wanavyofikisha neno la Mungu kwenye maeneo yanayowazunguka.”Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea” (1Wathesalonike 1:8). Roho hii itaonekana ndani ya wale wanafunzi leo ambao wanaamini na kutii Injili. Watawaambia wengine juu ya tumaini la ajabu ambalo Mungu ametoa kupitia Yesu Kristo, na kuwasaidia katika kuelewa ujumbe wa Biblia.

 

KUWA MWANAFUNZI MWEMA LEO.

Uanafunzi wa Bwana Yesu Kristo leo upo juu ya kanuni zile zile kama ilivyokuwa katika siku za Yesu. Neno “Mwanafunzi” kimsingi humaanisha yule anajifunza na kufuata wazo la yule anayefundisha. Aliachi tu wazo la kupokea maelekezo bali pia kujifunza kufanya kwa ajili ya nafsi yake kile ambacho mwalimu .amefundsha Hulaumu kufuata mufano uliowekwa na mwalimu na Bwana likuwa mwlimu mkuu zaidi ulimwengu kuwahikumona. Hakutarajia chochote zaidi ya wale waliotaka kumfuata kujiweka wakfu (Luka 14:25-33) kwa maana uanafunzi unahitaji badiliko katika maisha yetu.Tunaona katika maisha ya watu kama vile Petro na Paulo kwamba walimfuata kwa furaha na kwa hili ni mifano mikubwa san kwetu sisi.

 

Uanafunzi leo huhitaji maisha ya kila siku ya kufuata mafundisho na mfano wa Bwana wetu katika njia zetu zote Wanafunzi wana faraja kushiriki mwenendo wao na wengine waliona imani sawa kwa kukutana nao ili kumwabudu Mungu na kujadili Biblia pamoja kwa njia hii wanaweza wakusaidiana kujianda kwa ajili ya ile siku tukufu Bwana atapo kuwa akirudi kutoka mbinguni kuja kuwalipa watumishi wake waaminifu. Kwa wale ambao kwa uvumilivu na uaminifu walimtumikia katika kutokuwepo kwake atasema, njooni mlio banwa na Baba yangu, urithi ufalme mliowekewa tangu kuumbwa kwa ulimwengu (Mathayo 25:34)

 

Zingatia: Kijitabu cha bure cha msomaji wa Biblia kinapatikana, ambamo orodha ya uratibu na usomaji umetolewa ili kusaidia kusoma Biblia kwa mpango maalum. Ratiba hii itakufanya upitie Agano la kale mara moja na Agano jipya mara mbili kwa mwaka.Kuna maelfu wengi popote Duniani ambalo kila siku kufuata ratiba hii na kuona kuwa ni msaada mkubwa. Tafadhali tuandikie au omba kama unahitaji nakala.

 

MUHTASARI

* Dhamira kuu za msingi za ujumbe Injili ni:-

 1. Mambo yahusuyo Ufalme wa Mungu na

 2. Mambo yahusuyo jina la Yesu kristo (Matendo 8:12)

 

Kuamini na kutii Injili mtu ni lazima aelewe kweli za Biblia (Marko 15:16-16)

 

 • Mitume waliwa kubali tu wale walioamini na kutii injili kwa kubatizwa katika jina la Yesu kristo- hawa ndio waliokubaliwa kuingia katika jumuiya waumini (Matendo2:37-38,8:43-48)

 • Ubatizoni utambulisho wa hadhara wa mauti ya Yesu Kristo na ufufuo, na wa kile ambacho Mungu alikikamilisha ndani yake [Warumi 6:1-7].

 • Kwa kuomba ubatizo muumini atakiri kuwa yeye ni mwenye dhambi na hukiri kwamba anapaswa kufa. Anapotoka nje ya maji ya ubatizo huanza njia mpya ya maisha katika Kristo [Warumi 6:4-6, Wagalatia 2:20, Waefeso 4:22-24]

 • Maisha mapya ambayo sasa mwanafunzi huishi yanaelezwa naPaulo katika Wakolosai 3:1-17.

 • Usomaji wa kila siku na kufuata neno la Mungu ni nidhamu ya juu katika maisha ya Kristo [Yohana 6:63,Zaburi 1, Zaburi 119:97, 105, Petro 1:23-25]

 • Mwanafunzi hupenda kuzungumza na wengine kuhusu ukuu na maajabu ya Mungu yaliyofunuliwa katika Biblia [Malaki 3:16-17].

 • Maombi na shukrani huwa ni sehemu muhimu ya maisha ya kila siku ya mfuasi wa Yesu [Wafilipi 4:6,Wakolosai 4:2]. Hukubali kwamba Kristo yuko katika mkono wa kuume wa Mungu, akifanya upanisho kwa ajili yake [Waebrania 7:25, Warumi 8:34, 1Yohana 2:1-2,1:9]

 • Mwanafunzi ni “ndugu” au “dada” wa Bwana Yesu Kristo na ni sehemu ya familia ya Mungu aliye hai humkiri Mungu kama “Baba”yake [Mathayo 6:9]

 • Wote wafuasi wa kweli na Yesu ni viungo vya familia yote ya “mwili wa Kristo” nahukiri yeye kama “kichwa” kwao [waefeso 1:22-23]. Mwili huu umeungana Kwa kifungo cha upendo [waefeso 4:16, wakolosai 3:12-17].

 • Kuna kifungo cha ajabu cha ushirika na uangalizi wa kila mmoja ka mwenzake ambacho hujitokeza popote duniani katika mwili wa Kristo, yaani eklezia [Yohana 13:34-35].

 • Mfuasi wa Yesu anatakiwa kuzitunza amri zake na kufuata mfano wake katika mambo yote [Yohana 14:21]

 • Mfuasi waKristo atajitenga mwenyewe kutoka katika njia zisizo za kimungu za ulimwengu huu, hata fuata tama zake bali atafanya juhudi kuwa mtakatifu kimawazo na kivitendo [2wakorintho 6:14-17, 1petro 1:15,16]

 • Mfuasi wa Kristo hatajiingiza katika shughuli za kisiasa na kijeshi za ulimwengu huu [mathayo 5:39-44, 26:52, Danieli 4:17].

 • Mfuasi wa Kristo kwa furaha atawaambia wengine ili waamini injili ya ufalme wa Mungu ujao na njia ya wokovu kutoka katika dhambi. Atawaambia kuhusu tumaini hili kuu kama lilivyofunuliwa katika Biblia [2Timotheo 4:1-2].

 • Akizifuata amri za Bwana wake, mwanafunzi wa Yesu atakutana na wenzake kila juma ili kumkumbuka kwa kuumega mkate na kunywa divai [mathayo 26:26-29, 1wakorintho 11:23-29]

 

SOMO LA 26-MASWALI

  1. Ni zipi dhamira kuu mbili za Injli?

  2. Mtu anapoiamini Injili, kisha ni lazima afanye nini?

  3. Katika warumi 6:2-7, Paulo anasema kwamba kupitia ubatizo ‘Utu wetu wa kale’ umesulubiwa na tunapaswa ‘kuenenda katika upya wa uzima. Hii ina maanisha nini?

  4. Kwanini ni muhimu kwa mfuasi wa Yesu kusoma Biblia kila siku?

  5. Kwanini maombi yawe sehemu ya muhimu ya maisha yetu katika Kristo?

  6. Ikiwa Kristo ni “kichwa”jumuiya ya waumini ulimwenguni hufananishwa na nini?

  7. Kwanini wafuasi wa Yesu hujitenga na ulimwengu na njia zake?

  8. Kwasababu wafuasi wa Yesu sasa ni viungo katika familia ya Mungu kupitia Kristo, wanaitana vipi wenyewe kwa wenyewe?

  9. Kwanini wanafunzi wa Kristo hawajiingizi katika shughuli za kisiasa na kijeshi za ulimwengu huu?

  10. Yesu aliwaambia nini wanafunzi wake kufanya kwa ukawaida ili kumkumbuka yeye

 

Swahili Title: 
UANAFUNZI NDANI YA KRISTO LEO
English files: 
Swahili Word file: 
PDF file: