LIVING THE TRUTH Practical Principles for my Life in Christ. KUISHI KATIKA ILE KWELI Mwenendo wa kufaa kwa maisha yangu katika Kristo KUISHI KATIKA ILE KWELI MWENENDO WA KUFAA KWA MAISHA YANGU KWA KRISTO Upendo wangu kwa Mungu, na Mwokozi wangu Yesu Kristo 1. Yanipasa kumpenda Bwana Mungu wangu kwa moyo wangu wote na roho na akili na nguvu. Hii ni amri ya kwanza iliyo kubwa, kwa kuwa zote zinazofuata zimejumuishwa katika hii. Marko 12:30 2. Yanipasa katika maisha yangu kumtumikia kwanza Mungu. Hakuna kingine kilicho muhimu zaidi. Mathayo 6:33 3. Haja yangu ya daima itakuwa kufanya kazi zote za Bwana kwa uaminifu na bidii iwezekanavyo. Mathayo 24:45-47; Mdo. 20:28 4. Yanipasa kumwogopa Yeye atakaye wateketeza kabisa wasiotii na wasio waaminifu. 2 Thes. 1:7-9; Mathayo 10:28; 25:30 Ibada yangu na Ikelezia 5. Yanipasa kuwa mwaminifu katika kumkumbuka Yesu kwa Kumega Mkate kila juma. Hakuna kizuizi bali kukosa uwezo ndiko k utanikosesha ibada hii. Mathayo 26:26,28; 1 Wakorintho 11:23-26; Mdo. 2:42; 20:7 6. Nitakuwa katika mkutano mapema na kuona kwamba mkutano ukianza mara moja. Uzembe ni hali ya kutomweshimu Kristo. Warumi 12:11; 1 Wakorinto 14:40 7. Nitakutana na Ndugu na Dada zangu kwa furaha, kirafiki na salamu ya kuchangamka. Yohana 13:34; Warumi 12:10; Waefeso 5:2; Waqko losai 3:14; 1 Thes. 4:9 8. Katika huduma zote nitajaribu kukaza fikira kwa wepesi wa akili juu ya yote yanayosemwa na kufanyika. 1 Wakorintho 10:31; 11:29 9. Kama inatakiwa kutoa sala katikati ya watu, nitatoa sala kwa unyenyekevu na kwa lugha iliyorahisi kueleweka. Waefeso 6:18; Wafilipi 4:6; Wakolosai 4:2; Muhubiri 5:2 10. Kutoa changizo kwa wingi katika ikelezia, ni kumtolea Bwana. 2 Wakorintho 8:12-15; 9:6,7 11. Nitaweka bidii yote iwezekanayo na kushughulika katika maandalizi yangu ya kazi za ikelezia. 1 Timotheo 4:12-16; 2 Timotheo 2:15. Ibada yangu binafsi. 12. Yanipasa kusali mwenyewe, kila asubuhi na usiku iwavyo vyote. Luka 18:1; Mathayo 7:7; 6:9-13. 13. Yanipasa kumshukuru Mungu kwa kila jambo, hata kwa vitu vya kawaida, na kutamka sala fupi kwa kila mlo. Waefeso 5:20; Wakolosai 3:15-17; 1 Wakorintho 5:18; Waebrania 13:15. 14. Yanipasa kusoma Maandiko kwa kuyatafakari sana kila siku, huku nikimfikiria Mungu na kumwomba anisaidie kuyaelewa vema. Yahona 5:39; Mdo.17:11; 20:32. 15. Kwa kujifunza idadi ya maneno ya Biblia, nitaweza mwenyewe kumshuhudia Kristo katika mazungumzo ya kila siku. 1 Petro 3:15; Wakolosai 4:6. Wajibu wangu kwa kila mtu 16. Kujua jinsi wema wa Mungu nisivyostahili ulioonyeshwa kwangu, inanibidi siku zote kuwa mwema kwa wengine, hata kama nafikiria hawastahili.. Mathayo 5:44-48. 17. Siku zote yanipasa kuwa tayari kuwasaidia wenye shida nikimkumbuka Msamaria Mwema Luka 10:30-37; 1 Yohana 3:17; Yakobo 2:15,16. 18. Yanipasa kuonyesha upendo kwa wagonjwa na aliyezeeka, kwa asiye na baba na mjane, hasa walio katika ikelezia. Warumi 12:13; 2 Wakorintho 9:6-8; Waebrania 13:16. 19. Siku zote nitalipa ankara zangu. Warumi 13:8. 20. Sintojaribu kumshurutisha yeyote kunirudishia mali yangu iliyoazimwa au kuibiwa. Luka 6:35 21. Nitawaombea hata walio adui zangu, iwe katika mambo makubwa au madogo. Nitajibu mwenendo wao mbaya kwa wema. Luka 23:34; Mathayo 5:44; 1 Wakorintho 4:12,13; 1 Petro 3:9; Warumi 21:21. 22. Kwa kufuata kielelezo cha Bwana wangu kinanizuia kutumia nguvu au vurugu za namna yo yote. Mathayo 5:39; 26:52; Warumi 12:17-19. 23. Ni kuwa mwema siku zote, hata nikiudhiwa sana, na kuepuka maneno yote mabaya. 1 Petro 3:8,9; Waebrania 12:14. 24. Shughuli zangu za kila siku zitakuwa nyoofu kabisa na haki. Sintojishughulisha na shughuli zenye matendo ambayo ni ya kawaida katika ulimwengu huu. Warumi 12:17. 25. Katika mambo yote inanibidi kuwafanyia wengine kama nipendavyo wanifanyie mimi. Mathayo 7:12. Wajibu wangu Mahususi kwa Ndugu na Dada zangu. 26. Nitajaribu siku zote kuona mema kwa wengine na si mabaya. Mathayo 7:12; Luka 6:41; 1 Wakorintho 13:4,5. 27. Haitakiwi kukasirika kwa urahisi, bali kukumbuka ni kiasi gani nimesamehewa na Mungu. Mathayo 5:23,24; Wakolosai 3:12-14. 28. Nitakubali kukemewa kwa ustahimilivu na kunyenyekea. Waebrania 13:22; 12:1-11; 2 Wakorintho 7:8-11. 29. Yanipasa kuwa tayari kusamehe kwa moyo wangu wote kosa lo lote juu yangu. Mungu hatanisamehe isipokuwa nami nikifanya hivyo. Mathayo 18:21, 22, 35; Waefeso 4:31,32. 30. Ugomvi na kulaani kusiwe na sehemu katika maisha yangu katika Kristo - ni ulimwengu tu ndio hufanya mambo ya jinsi hii. Tito 3:2; 2 Timotheo 2:24. 31. Natakiwa kuchukua tahadhari ya kwamba ndugu walio dhaifu na wachanga katika Kristo hawakwaziki kwa lo lote nifanyalo au kusema. Warumi 14:13, 21; 1 Wakorintho 8:13; Mathayo 18:6. Mahusiano kwa Rafiki na Jamaa zangu. 32. Ninatakiwa kuwa makini kuhusiana na watu ninaoongozana nao. Baadhi ya rafiki watanisaidia, lakini wengine watanizuia katika juhudi yangu kumfuata Kristo. 1 Wakorintho 15:33; 5:6; Wafilipi 4:8. 33. Nitawataka wa kufuatana nami katika ushirika ambao ni ndugu na dada, nitachagua marafiki katika ikelezia. 1 Petro 4:3-5; Waefeso 5:6-8; Mdo.2:42; Waebrania 10:24-25. 34. Yanipasa kuepuka uasherati na uzinzi, hata kama ulimwengu unaona ni mambo ya kawaida. Ngono nje ya ndoa ni chukizo mbele za Bwana na ni kuushushia hadhi mwili wangu, ambao naona kuwa ni hekalu la Mungu. Yanipasa kuwaambia rafiki zangu watakao kunijaribu ya kwamba sitaki kuwa na maisha ya aina hiyo. 1 Wakorintho 5:9-11; 6:13,18, 19; Waefeso 5:3; 1 Wathesalonike 4:3; Math 5:28. 35. Iwapo mimi sijaoa, utakatifu na uaminifu kwa Kristo unataka kwamba kuoa katika Bwana. Itakuwa ni upumbavu kwangu kutia nira maisha yangu na mwenza asiyeamini. 1 Wakorintho 7:39; 2 Wakorintho 6:14. 36. Kama mimi ni mume, nitakuwa mwema na mpole kwa mke wangu, sio kumnyima mapenzi yangu kwake, kama Kristo alivyojitoa mwenyewe kuwa dhabihu kwa kanisa. Waefeso 5:25; Wakolosai 3:19; 1 Petro 3:7. 37. Mimi kama ni mke, nimkiri mume wangu kuwa ni kichwa cha jamaa, kama kanisa linavyojitiisha na utii kwa Kristo Bwana wake. Waefeso 5:22-24; Wakolosai 3:18; 1 Petro 3:1. 38. Talaka isifikiriwe: "Alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asitenganishe". Mathayo 19:4-6; 1 Wakorintho 7:10,11. 39. Mimi nikiwa mzazi, kamwe sintapumzisha juhudi yangu katika kuwafunza watoto wangu maarifa ya Injili na tabia nzuri. Nitachukua hadhari ya kwamba siwafanyi watoto wangu kuwa wenye hasira na wanavyotendewa nyumbani. Waefeso 6:4; Wakolosai 3:21. 40. Kama mwana au binti, nitakuwa mtiifu kwa wazazi wangu, iwe wapo katika Bwana au la, isipokuwa wakiniambia kufanya kinyume na maagizo ya Kristo. Nitawapa heshima ya kufaa na sio kuwarudishia kauli mbaya. Waefeso 6:1,2; Wakolosai 3:20. Kazi yangu ya kila siku. 41. Nikiwa mwajiri, nitakuwa mwema, mwenye haki na mpole kwa wafanyikazi wangu na watumishi. Wakolosai 4:1; Waefeso 6:5. 42. Nikiwa nimeajiriwa na wengine, nitatumika kwa bidii na uaminifu. Bado yanipasa kufanya hivi hata mwajiri asipotoa kile ninachofikiria kuwa ni haki au ujira wa haki. Wakolosai 3:22-25; Waefeso 6:5. 43. Hainipasi kujisaidia mwenyewe katika mali ya mwajiri; sitachukua hata kitu kilicho kidogo zaidi pasipo kuomba kwanza. Tito 2:9,10; Wakolosai 3:22-25. Mambo ya Msingi kwa uhai wa Ikelezia langu. 44. Nitaiga mifano bora niijuayo katika ikelezia. 1 Wakorintho 11:1; Wafilipi 3:17; Waebrania 13:7. 45. Siku zote nitasaidia kuhubiri Injili kwa kila namna niwezavyo, hasa kwa kusaidia mikutano yote. Nitazungumza na wengine kwa uhuru katika kila nafasi juu ya tumaini nililonalo na lenye thamani kwangu Luka 12:8; Marko 8:38; 2 Timotheo 1:8. 46. Natakiwa kujihadhari na waalimu wa uongo na kupima yote nisikiayo kwa Neno la Kweli. 1 Wathesalonike 5:21; 2 Petro 2:1; Mathayo 24:24. 47. Kulaumiana na kunung'unika huleta huzuni sana. Kama jambo fulani ni baya sana ambalo naona siwezi kulipuuzia au kulisahau, inanibidi kusema na mtu mhusika. Hajali, inanibidi niende tena na mshauri. Kama hakuna maendeleo yo yote, wakati huo nitaweka hilo suala mbele ya ikelezia. Wafilipi 2:14,15; Mathayo 18:15-17. 48. Iwapo ninatunza chuki au hasira dhidi ya awaye yote, kuacha kwenda Kumega Mkate sio suluhisho. Njia pekee ni kumwomba Mungu aondoe hasira katika moyo wangu. 1 Wakorintho 4:5; Yakobo 3:14,15; 1 Yohana 4:20,21. 49. Ninapokosea katika lo lote, inanibidi kukiri kwa hiari na kuomba msamaha. Yakobo 5:16; Zaburi 32:5. 50. Ugomvi hautakiwi kuingia katika ikelezia langu. Sote ni jamaa moja katika Bwana, Hata mawazo yaliyo na uchungu ni mabaya. Waefeso 4:29,31, 32; Wakolosai 4:6; Tito 2:7,8. 51. Nitasaidia kuzuia kuunda migawanyiko au vikundi katika ikelezia. Je! Kristo amegawanyika? 1 Wakorintho 1:12,13; 3:3,4; Wafilipi 2:1-3. 52. Hakuna taifa au tofauti ya watu katika Kristo. Jambo hili Mungu analichukia. Wagalatia 3:28; Ufunuo 7:9; Mdo. 10:34, 35; Yakobo 2:8,9. Kujilinda mimi mwenyewe na Ulimwengu 53. Siku zote nitajiepusha na mambo yenye kuzua mawzo mabaya - picha mbaya, magazeti, au vitabu au aina yo yote ya mazungumzo yasiyofaa. Wafilipi 4:8; Waefeso 5:3,4; Warumi 1:28-32; 1 Petro 2:11. 54. Maneno yangu yatakuwa mbali na kukufuru na lugha mbaya. Mungu anasikia kila neno langu. Mathayo 5:37; 12:36. 55. Kuteta na kusingizia ni maovu makubwa, nami nitaepuka yote. Tito 3:2; Waefeso 4:31,32 56. Majivuno na kutokuwa mwaminifu hata katika mambo madogo ni kosa. Yanipasa kuyaweka mbali na maisha yangu. Tito 1:10; 1 Petro 2:1,21,22; Mdo.5:1-11; Ufunuo 22:15 57. Nisimpeleke yo yote mahakamani. Huu ndio mwenendo wa ulimwengu. Tabia ya Kristo ni kukubali baya. 1 Wakorintho 6:1-7; Mathayo 5:38-42 58. Nikiwa mfuasi wa Kristo, siwezi kuwa na nafasi au kushiriki katika chaguzi na siasa za ulimwengu, kwa kuwa siasa maana yake ni kuwatumainia wanadamu - nami imani yangu itakuwa kwa Mungu na Ufalme wake ujao. 2 Wakorintho 6:14-18; 1 Petro 2:11,12; 1 Yohana 1:6; 2:15; Yohana 18:36 59. Maadam maisha yangu kipaumbele ni kwa Kristo, na nimeamriwa kuishi kwa amani na watu wote, sitakiwi kujiunga na jeshi au polisi au kushiriki shughuli yo yote ya kijeshi. Mathayo 26:52; Yohana 18:36 60. Nikiwa mfuasi wa Kristo, sintakuwa na sehemu katika vyama vya kindugu au ushirika wo wote wa jinsi hii. Tuna ushirika mkubwa usio wa ulimwengu huu. 1 Wakorintho 10:20,21; 2 Wakorintho 6:14,15; 1 Yohana 1:3 61. Yanipasa kujilinda na tamaa za ulimwengu na dhidi ya matokeo yake mabaya juu ya maisha yangu ya kiroho na utumishi wa ikelezia. 1 Timotheo 6:10; 2 Timotheo 3:1,2 62. Ulevi ni mbaya nao umekatazwa. Siku zote akili yangu itakuwa wazi na kuwaza mambo matakatifu na si kujichafua na ulevi. Warumi 13:13,14; 1 Wathesalonike 5:6,7; Waefeso 5:18 63. Yanipasa kutunza sheria za nchi yangu kwa uangalifu sana na kujiepusha kufanya makosa, katika madogo na mambo makubwa vilevile. Ni pale tu ninaposisitizwa kutenda kinyume na Kristo hapo ni haki yangu kutotii. Warumi 13:1-7; 1 Petro 2:13,14; Tito 3:1 Kufanya Maisha yangu kuwa Matakatifu mbele za Mungu 64. Siku zote natakiwa kushindana na tamaa za mwili, na sitakubali mwenyewe kukatishwa tamaa kwa hila na tabia ya walionizunguka. Wagalatia 5:16,24; 2 Timotheo 2:22; Yakobo 1:3,4 65. Ni vibaya kukasirika upesi. Kama nikiwa hivyo, yanipasa kuitawala. Yakobo 1: 19,20; Mithali 16:32; 19:11 66. Inanibidi kusema ukweli siku zote. Kudanganya ni uovu mkubwa. Matokeo ya uongo wa nyoka katika Edeni hata sasa yapo nasi. Waefeso 4:25; Wakolosai 3:9; Mdo.5:1-11; Ufunuo 22:15 67. Yote nifanyayo na kusema yaonyeshe kwamba mimi ni mfuasi wa Yesu, na siku zote nitajilinda dhidi ya kumkana. Luka 12:8; Marko 8:38; 2 Timotheo 1:8 68. Sitakiwi kuwaonea husuda walio na maisha mazuri kuliko yangu. Luka 12:15; Mathayo 6:19; Waebrania 13:5 69. Nitamkiri Baba kwa mwongozo na ukuu katika maisha yangu kwa kusema, "Bwana akipenda", "Mungu akipenda", Kwa neema ya Mungu". Yakobo 4:14,15; Mithali 3:6 70. Siku zote nitamweka Yesu moyoni mwangu. Hata nikikabiliwa na shida, nitajiuliza "Yesu atafanyaje?" 2 Petro 2:21-23; Yohana 13:15 71. Katika mambo yote lengo liwe katika usafi na utakatifu, na hivyo kumpendeza Bwana aliye mbinguni. Warumi 6:19,22; 1 Yohana 3:3; Waebrania 12:14 72. Ninaamini kurudi kwa Bwana wangu kumekaribia. Yanipasa kuishi kama mtu aaminiye kwa kweli. Mathayo 24:44; 10:37,38; Luka 12:35-37; 2 Petro 3:13,14 Jinsi Mungu atakavyonisaidia 73. Kamwe nisiridhike na juhudi yangu kumpendeza Mungu. Mimi ni dhaifu kuliko ninvyokubali. 1 Wakorintho 10:12; Warumi 5:12; 7:18-25 74. Kwa mara nyingi nitamwomba Mungu anitie nguvu ili kwamba nifanye vyema. Msaada mkubwa utapatikana kwa wale wautakao. Wafilipi 4:6,13; Yakobo 1:5,6; 2 Wakorintho 12:9; Waefeso 3:16 75. Hata kama nimekuwa dhaifu na kukosea vibaya sana, sintokatishwa tamaa na kuacha. Kama kweli nikisikitika kweli kweli kwa kile nilichofanya, na nikikusudia kurekebisha mwendo wangu hapo baadaye, Mungu atanisamehe na kunisaidia kujaribu tena. Luka 15: 11-32; 2 Wakorintho 7:10; 1 Yohana 1:9.